Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wanawake,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na uongozi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kabla ya kikao cha Mene4jimenti ya Mfuko huo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wanawake,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akimzikiliza Mkurugenzi wa NHIF Bw. Bernald Konga kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wanawake,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akizungumza na uongozi huo..
Mkurugenzi wa NHIF Bw. Bernald Konga akiandika baadhi ya mambo wakati Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wanawake,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu alipozungumza nao.
…………………………………………………………………………………….
Na.WAMJW,DSM
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imetakiwa kutatua malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa wananchi wenye bima ya afya.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kikao na Menejimenti ya Mfuko huo katika ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini, Dar es Salaam.
“Kumekuwepo na malalamiko ya upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa watu wenye kadi za bima pia ucheleweshaji wa malipo ya watoa huduma za afya” Alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ameutaka mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa katika vifurushi vya bima ya afya.
“Tatueni malalamiko yote kwa wakati ili wananchi wafurahie vifurushi vyote watakavyojiunga navyo”.Alisisitiza Waziri Ummy
Kikao hicho pia kiliangalia mwenendo wa utoaji wa huduma za bima za afya zinazotolewa na mfuko huo ambapo kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Benard Konga, Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, na Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi.