Home Mchanganyiko NDALICHAKO AZINDUA VETA NYAMIDAHO KIGOMA

NDALICHAKO AZINDUA VETA NYAMIDAHO KIGOMA

0

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikata utepe kushiria uzinduzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Nyamidaho kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiangalja baadhi ya vifaa vya kisasa vya ujenzi vinavyotumika kufundishia katika chuo kipya cha VETA Nyamidaho wakati wa uzinduzi wa chuo hicho

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiweka udongo kwenye mti wa kumbukumbu alioupanda wakati wa uzinduzi wa chuo cha Ufundi Stadi Nyamidaho

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiangalia moja ya nguo ilioshonwa na wanafunzi wa chuo kipya cha VETA Nyamidaho wakati wa uzinduzi wa chuo hicho

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akijaribu moja ya mtambo wa kisasa wa kufyatulia matofali unaotumika kufundishia katika chuo cha ufundi stadi Nyamidaho

Moja ya jengo lililojengwa katika Chuo Kipya cha Ufundi Stadi Nyamidaho kilichozinduliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako

……………………………………………………………………………………………..

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amezindua Chuo cha Ufundi Stadi Nyamidaho kilichopo Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Profesa Ndalichako amesema uanzishwaji wa Chuo hicho ni mwendelezo wa utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga vyuo vya ufundi stadi katika kila Wilaya Nchini ili kupeleka huduma hiyo karibu na Wananchi na kuwapatia ujuzi vijana wa kitanzania.

Ndalichako amesema Chuo cha Nyamidaho kimetokana na majengo yaliyokuwa yakitumiwa na Taasisi ya World Vision ambapo Serikali imekarabati majengo yaliyokuwepo na kujenga mengine mapya.

Waziri Ndalichako ameeleza kuwa jumla ya Shilingi milioni 534 zilitolewa kwa ajili ya kazi hiyo na kwamba zimetumika milioni 477 hadi ukamilishaji. Aidha ameridhia ombi la kiasi kilichobaki kutumika kuanzisha ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kiume.

Ameongeza kuwa katika Mwaka 2019/20 vyuo 10 vya Halmashauri za Wilaya vimejengwa na kuanza kutoa mafunzo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga ameishukuru Wizara ya Elimu kwa kukamilisha ujenzi wa chuo hicho na amewataka wakazi wa kijiji cha Nyamidaho kuhakikisha vijana wao hasa wa kike wanajiunga na chuo hicho.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya VETA, Peter Maduki ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuimarisha Elimu ya Ufundi nchini na kuongeza kuwa Chuo hicho kipya kina wanafunzi takriban 70. Aidha ameagiza Uongozi wa VETA kutoa bure mafunzo ya kozi ya uwashi kwa wanafunzi wanaotoka Nyamidaho.