Home Mchanganyiko SUA watembelea Makumbusho ya Taifa kujifunza

SUA watembelea Makumbusho ya Taifa kujifunza

0

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine wanaosomea masomo ya Utalii wakipimwa joto kabla ya kuingia Makumbusho. Wanafunzi hao walitembelea makumbusho kwa lengo ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu utalii na uhifadhi.

Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa Bibi Anamery Bagenyi akitoa maelezo kuhusu nyayo za mwanadamu wa kale zilizogundulika huko Laetoli katika Bonde la Olduvai.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro wakimsikiliza Afisa Elimu, Bibi Magreth Kigadya akitoa maelezo kuhusu Sanaa za sasa zilizopo Makumbusho ya Taifa. Wanafunzi hao wako katika ziara ya mafunzo jijini Dar es Salaam.

Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu ch Sokoine kuhusu chimbuko la mwanadamu na zana za mawe wanafunzi hao walipotembelea Makumbusho kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na masomo yao.

Afisa wa Makumbusho ya Taifa Bw. Ayubu Madenge akitoa maelezo kuhusu historia ya Tanzania kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine Morogoro walipotembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza.

****************************

Na Mwandishi Wetu

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) wanaosomea fani ya Utalii (Tourism Management) wametembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam kujifunza mambo mbalimbali yanahusu utalii.

Wanafunzi hao ambao wako mwaka wa pili wa masomo yao wamefika Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo mikusanyo, maonesho na vifaa mbalimbali vinavyotumika katika maonesho.

Wanafunzi hao wapatao 203 walifika pamoja na walimu wao wawili ambapo waliweza kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo kumbi za historia, chimbuko la mwanadamu, michoro ya miamba, Sanaa za sasa na baiolojia.