Home Siasa MAKUNGU AJITOA KUPEWA RIDHAA YA KUWANIA URAIS ZANZIBAR

MAKUNGU AJITOA KUPEWA RIDHAA YA KUWANIA URAIS ZANZIBAR

0

………………………………………………………………….

 Mwanachama wa CCM, Hussein Ibrahim Makungu amekuwa mtia nia wa kwanza kujitoa katika kinyang’anyiro hicho baada ya kujitokeza kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya urais Zanzibar majuma mawili yaliyopita.

Makungu amesema, amefikia uamuzi huo ili kutoa nafasi kwa watia nia wengine kuendelea na mchakato huo na kukipunguzia chama chake cha Mapinduzi kazi ya kuchuja wanachama wenye sifa ya kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar.