Home Siasa TUTAWANG’OA WENYE KUTOA RUSHWA MAKAMU WA RAIS AONYA

TUTAWANG’OA WENYE KUTOA RUSHWA MAKAMU WA RAIS AONYA

0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd akiongea  wakati wa ziara yake ya kichama Mkoani Shinyanga alipokutana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa na Wilaya ya Kahama kama mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akiongea akifuatilia kwa makini hotuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd wakati wa ziara yake ya kichama Mkoani Shinyanga alipokutana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoani humo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd akiongea  wakati wa ziara yake ya kichama Mkoani Shinyanga alipokutana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa na Wilaya ya Kahama kama mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga.

……………………………………………………………………………

Na Mwandishi wetu Shinyanga

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd amewaonya baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chama hicho kujiepusha na matumizi ya fedha katika kutafuta nafasi za uongozi kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba ya Chama hicho.

Aidha Barozi Seif Ali Idd ameonya kuwa kuna baadhi ya watu wenye nia ya kugombea uongozi lakini badala ya kwenda wenyewe wanatuma watu wengine kutoa rushwa kwa niaba yao nakuonya kuwa wana taarifa zao na watashughulikia ipasavyo kwani watu wanonunua uongozi sio watu wazuri hata kidogo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kichama Mkoani Shinyanga alipokutana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa na Wilaya ya Kahama kama mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga.

‘’Kiongozi yoyote anayetafuta uongozi kwa kwa kununua huyo sio kiongozi mzuri, uongozi hautafutwi kwa kununua bali uongozi utafutwa kwa kujenga hoja’’. Aliendelea kusema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd.

Aidha Kiongozi huyo mkubwa Nchini amesisitiza kuwa serikali iko macho sana kuwabaini wale wote wanaotaka kutumia ushawishi wa fedha kujipatia uongozi kwani macho yake yanaangaza  kila mahali na wana uhakika kuwa wataonekana pasiposhaka na kuwataka kuacha siasa za namna hiyo mara moja.

Barozi Seif Ali Idd amesema mtu akiwaletea viburungutu vya fedha kwa lengo la kununua uongozi chukueni lakini msiwachague maana unaweza kukosea kuchagua na ukajikuta unachagua uhalifu katika jimbo kwani kiongozi anayechaguliwa kwa rushwa ni mhalifu kama walivyo waalifu wengine.

Aidha Barozi Idd amewataka wabunge Mkoani Shinyanga kuendelea na kazi ya kukamilisha ahadi zao kwa wananchi kwani bado ni viongozi mpaka zoezi lakuchukua fomu litakapoanza ingawa inawezakena baadhi yao wanaweza kuwa wanamaliza muda wao na wengine kupoteza nafasi za uongozi kwa kushindwa katika kura za maoni.

 ‘’Achaneni nao viongozi wanaotumia fedha kutimiza ahadi ya chama cha mapinduzi ambayo inataka mgombea kupita bila matumizi ya rushwa na tamaa. Ukumpitisha kiongozi wa rushwa maana yake umepitisha uovu kwenye jimbo’’. Alionya Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Idd.

Aidha kiongozi huyo ameonya kuwa kwasasa kuna baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na baadhi ya watu serikalini wanaojifanya madalali wa wagombea na  wanawahamasisha baadhi ya watu kwenda kugombea nafasi ya uongozi na kuonya kuwa tabia hii pia haikubaliki kwani uongozi ni suala la hiari.

Katika salam zake kwa wanachama wa chama cha Mapinduzi Mkoani Shinyanga Mbunge wa Kahama Jumanne Kishimba amemwomba Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd kuangalia namna bora ya kuwapa motisha hata kuwapatia Bima za Afya kutokana na juhudi zao katika kujenga Chama Cha Mapinduzi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar yuko Mkoani Shinyanga kwa ziara ya Kichama na ataendelea ziara yake katika Manispaa ya Shinyanga na kuendelea kufanya shughuli za Chama kwa kuwa ni mlezi wa Chama hicho Mkoani Shinyanga.