Home Burudani MSANII WA NIGERIA OLAKIRA KUACHIA WIMBO MPYA WA  ‘IN MY MASERATI’

MSANII WA NIGERIA OLAKIRA KUACHIA WIMBO MPYA WA  ‘IN MY MASERATI’

0

******************************

NA MWANDISHI WETU.
MSANII nyota wa miondoko ya Afro Pop, Pop na RnB kutoka Nchini Nigeria, Adefemi Ebenezer maarufu kama Olakira   Ijumaa ya 26 Juni anatarajia rasmi kuachia wimbo mpya wa ‘In my Maserati’.
Olakira anayetamba na nyimbo bora mbalimbali zikiwemo  ‘Aya Mi’,  ‘Wakanda Jollof na zingine nyingi ambapo kwa sasa anakuja ba ujio mpya wa wimbo wake utakaokuwa kwa sauti na video ‘In my Maserati’.
“Wimbo wa In my Maserati unaelezea namna anavyovutiwa na gari la kifahari aina ya Maserati akimuahidi mpenzi wake na kuliendesha gari hilo”
Wimbo huo umetayarishwa na Olakira mwenyewe huku video ikiwa imechukuliwa viunga vya Jiji la Lagos na kuongozwa na Clarence Peters.
Aidha, Msanii Olakira amekuwa akifanya vizuri kwenye tasnia ya muziki Nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla kwa kutoa muziki mzuri wa Afropop.
Ujio wake katika Afropop alianza na wimbo wa  ‘Hey Lover’  na baadae wimbo wa ‘Flirty signal’ ambapo zilipokewa vizuri na kupata watazamaji (views) wengi kupitia mtandao  wa Youtube.
Olakira pia ameshiriki kuandika na kuandaa wimbo uliofanya vyema katika Afro wa ‘Akube’ na ‘My Woman’ wa Dotman na kumuweka katika chat za juu kwenye ramani ya muziki Afrika.
Pia mbali na kuwa ni Mwanamuziki, Olakira ni Mtayarishaji wa muziki (Producer ),mwandishi wa mashahiri ya muziki (songwriter ).