Home Siasa DKT. HUSSEN MWINYI AREJESHA FOMU, ASUBIRIA MAAMUZI YA CHAMA

DKT. HUSSEN MWINYI AREJESHA FOMU, ASUBIRIA MAAMUZI YA CHAMA

0

*******************************

NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo 24 Juni, amerejesha fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Dkt. Hussein Mwinyi aliwasili majira ya saa nane mchana kurejesha fomu hiyo ambapo ilikaguliwa na kisha kwenda kuirejesha kwa Katibu wa Idara ya Organization CCM, Cassian Galos.

Hata hivyo aliweza kuzungumza kwa kifupi pekee ambapo alisema:

“Kwa sasa hatua ya kwanza mchakato umemalizika wa kuchukua fomu na kurejesha.

Ninachosubira ni maamuzi ya Chama. Wakiona nafaa sawa. Wakiona sifai sawa. Tutashirikiana na mwenzangu atakayepitishwa.” Alieleza Dkt. Hussein Mwinyi.

Pia aliongeza kuwa, Mpaka sasa idadi ya wagombea imeongezeka kutokana na kukua kwa demokrasia ndani ya chama ma kufukia 24″ alimalizia Dkt. Hussein Mwinyi.

Hata hivyo hadi kufikia leo 24 Juni, tayari Makada 26 wameshafika kuchukua fomu huku waliorejesha wakifikia 6.

Ambao ni pamoja na Husna Attai Masoud, Fatuma Kombo Masoud, Mwatum Mussa Sultan, Balozi Ali Karume, Mohammed Hija Mohammed, Mbwana Bakari Juma na Abdulhalim Mohammed Ali na Hamis Musa Omary.

Aidha hadi sasa watia nia wengine waliokwisha jitokeza ni pamoja:

Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Sheha Mussa, Shamsi Vuai Nahodha, Mohammed Jaffar Jumanne, Issa Suleiman Nassor, Prof. Makame Mnyaa Mabarawa na Haji Rashid Pandu.

Pia wamo:
Jecha Salum Jecha, Dk Dkt. Khalid Salum Mohammed, Rashid Ali Juma, Mmanga Mjengo Mjawiri, Hamad Yussuf Masauni, Mohammed Aboud, Bakar Rashid Bakari, Hussein Ibrahim Makungu, Ayoub Mohammed Mahmoud na Hashim Salum Hashim