Home Mchanganyiko BODI YA REA YAGOMA KUONGEZA MUDA KWA KAMPUNI YA A TO Z...

BODI YA REA YAGOMA KUONGEZA MUDA KWA KAMPUNI YA A TO Z INAYOTEKELEZA MRADI WA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI MKOA WA DODOMA

0

Mjumbe wa Bodi ya REA,Bw. Henry Mwalwinza akizungumza wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini katika kijiji cha Chilanjilinzi wilaya Kongwa mradi unaotekelezwa na Kampuni ya A to Z .

Meneja wa Kampuni ya A to Z ,Yasir Azmi,akitoa maelezo kwa Mjumbe wa Bodi ya REA Bw.Henry Mwalwinza (hayupo pichani) ambaye alifanya ziara ya kukagua mradi unaotekelezwa na kampuni hiyo Mkoa wa Dodoma.

Mafundi wa REA wakiendelea kufunga nyaya za umeme kwa ajili ya kusambaza umeme katika kijiji cha Chilanjilinzi wilaya Kongwa mradi unaotekelezwa na Kampuni ya A to Z .

Nyaya za umeme 

…………………………………………………………..

Na. Alex Sonna, Dodoma

Bodi ya Mradi wa Umeme Vijijini (REA) imegoma kuongeza muda kwa mkandarasi wa Kampuni ya  A to Z Infra LTD anayetekeleza mradi wa kusambaza umeme vijijini katika mkoa wa Dodoma ambaye muda wake unaisha Juni 30, mwaka huu.

Kauli hiyo ameitoa leo na Mjumbe wa Bodi ya REA,Bw. Henry Mwalwinza wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme katika kijiji cha Chilanjilinzi wilaya Kongwa mradi unaotekelezwa na Kampuni ya A to Z .

Aidha Mwalwinza amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo mpaka sasa wametekeleza kwa asilimia 61 ambayo ni kiwango cha chini kwani makubalianao ya mradi huo ilikuwa n miezi 24 ambayo kikomo chake ni Juni 30 mwaka huu.

Mwalwinza ameelez kuwa baadhi ya kazi zao ziko chini ya kiwango hivyo wanatakiwa kurekebisha kazi hizo kabla ya ukomo wa muda uliyo pangwa kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Naelekeza Miradi iliyobaki ikamilishwe kwa kiwango na ubora unaohitajika na hakikisheni mnatumia mafundi wenye ufanisi mzuri ili miradi hiyo kuwa katika ubora unao stahili”, ameelekeza Mwalwinza.

Mwalwinza ameongeza kuwa kampuni hiyo hisipo kamilisha mradi huo kwa muda uliyopangwa itachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwafikisha katika mamlaka husika ili hatua zaidi zichukuliwe.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya A to Z ,Yasir Azmi,awali akiwasilisha taarifa yake kwa wajumbe wa Bodi ya REA ameomba kuongezewa muda wa miezi miwili ili kukamilisha kazi hiyo na kukabidhi ikiwa katika ubora wake.

“Napenda kuihakikishia Bodi ya REA kuwa tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kuhakikisha tunakamilisha mradi hu una kukabidhi kwenu ukiwa katika ubora unaohitajika japo tayali tuko nje ya muda uliyopangwa”, ameeleza Mkandarasi wa Kampuni ya A to Z.