Home Burudani ZAMARADI “KUIBUA FURSA ZA WASANII KUSHIRIKI MAONESHO SABASABA KUMEKUCHA

ZAMARADI “KUIBUA FURSA ZA WASANII KUSHIRIKI MAONESHO SABASABA KUMEKUCHA

0

********************************

Na Magreth Mbinga

Mtangazaji na mjasiriamali, Zamaradi amekuja na Meet Your Stars kwaajili ya wasanii kuuza bidhaa zao kupitia maonesho ya Sabasaba ambapo wasanii ambapo wanabidhaa zao watapata fursa bure ya kuwa na banda kupitia kijiji hicho ambacho kitakuwa Sabasaba Temeke jijini Dar es salaam.

Aidha Zamaradi amesema hakuna msanii ambaye atalipishwa kuwa na banda kwani amezungumza na wahusika wa eneo la maonesho na wametoa eneo ambalo kwa sasa linaandaliwa kwaajili ya mabanda hayo.

Pamoja na hayo Zamaradi amewataka wasanii kuchangamkia fursa hiyo kwani itafungulia masoko mapya ya bidhaa zao kwa kuwa eneo hilo linakuwa na wageni wa aina mbalimbali.