Home Mchanganyiko RC OTHMAN ATOA ONYO KWA WALIMU WALIOTEULIWA KUSIMAMIA MITIHANI KIDATO CHA SITA

RC OTHMAN ATOA ONYO KWA WALIMU WALIOTEULIWA KUSIMAMIA MITIHANI KIDATO CHA SITA

0

…………………………………………………………………………

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman akifungua mafunzo ya walimu watakaosimamia mitihani ya kidato cha sita  yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kilichokuwa chuo cha uwalimu Benjemini Mkapa Wete 

Picha na Masanja Mabula

……………………………………………………………..

Na Masanja Mabula PEMBA.

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba   Omar Khamis Othman amewataka walimu walioteuliwa kusimamia mitihani ya kidato cha sita kufuata taratibu na sheria ili kudhibiti vitendo vya uvujaji wa mitihani.

Alisema jambo la kuzingatia wakati wa mitihani ni uwadilifu kwa wasimamizi kwa kutotoa mianya kwa wanafunzi kuingia ndani ya chumba cha mtihani na vitu visivyoruhusiwa.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na walimu walioteuliwa kusimamia mitihani ya kidato cha sita pamoja na wajumbe wa kamati za mitihani za mkoa huo.

“Kila mmoja anapaswa kusimamia uwadilifu ili kuhdibiti vitendo vya udanganyifu wakati wote wa  kipindi cha mitihani yao ya Taifa”alisema.

Mapema katibu wa kamati ya mitihani mkoa huo ndg Bakar Ali Bakar amesema kamati imejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wanafanya mitihani kwa amani na bila udanganyifu.

Alisema hawatakuwa tayari kuona vitendo vya udanganyifu vinatokea na kusababisha sifa mbaya kwa mkoa, hivyo atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.

“Kamati tayari imeweka mazingira mazuri yatakayowawzesha wananchi kutoingia na vitu visivyoruhusiwa kwenye chumba  cha mitihani”alieleza.

Kwa upande wake afisa kutoka Mamlaka ya kuzuia Rushwa na uhujumu wa uchumi zanzibar –ZAECA-Shuwekha Abdalla Omar alisema ZAECA ,imejipanga kukabiliana na vitendo vya udanganyifu.

Alisema tayari wamepeana  majukumu ya kupita karibu na maeneo ya skuli ambapo lengo ni kufuatilia suala zima ya ufanyaji wa mitihani kwa wanafunzi.

Jumla ya wanafunzi 206 wanatarajia kufanya mitihani ya kidato cha sita katika mkoa wa kaskazini pemba itakayoanza jumatatu ya tarehe 29 mwezi huu.