Home Mchanganyiko Pro. Kabudi Afungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri SADC Dar es Salaam

Pro. Kabudi Afungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri SADC Dar es Salaam

0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na waandishi wa habari (hawaako pichani), kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge baada ya kumaliza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao katika Katika
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano  (JNICC) jijini Dar es Salaam.

***********************************

 

Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC
uliofanyika kwa njia ya video umepitisha kwa kauli moja Mwongozo wa Kikanda wa Urazinishaji (harmonization) na uwezeshaji wa shughuli za usafirishaji ndani ya SADC wakati huu wa janga la Corona.

Akizungumza na wanahabari katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano  (JNICC) jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi amesema katika mkutano huo wamepitia wamepitia na kujadili masuala ya uratibu, usimamizi na uangalizi wa usafirishaji kwa njia ya barabara katika vituo vya kuingilia, ukaguzi dhidi ya Virusi vya Corona vinavyotambuliwa na SADC na namna ya kuendeleza shughuli za biashara wakati huu wa janga la Corona ili kunusuru uchumi na kupunguza umasikini ndani ya jumuiya.

“Tunaendelea kufanya biashara,tunaendelea kuruhusu bidhaa na huduma muhimu kupita katika nchi zetu lakini pia kuweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba tunazuia au kuhakikisha maradhi haya au janga hili la Covid-19 haliongezeki” Amesema Prof.Kabudi.

Aidha Prof.Kabudi amesema wamekubaliana kuwa na mpango wa pamoja wa kununua dawa, vifaa tiba na kinga kutoka nchini India na kuwa na hatua za pamoja za kukabiliana na ugonjwa wa COVID 19.

Mafanikio makubwa ambayo yamepatikana katika jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) usafirishaji wa bidhaa na huduma muhimu umeendelea hata wakati huu wa kipindi kigumu cha Maambukizi ya Virusi vya Corona.

“Kuna changamoto zimetokea na hazikukosa majawabu ama kati ya nchi na nchi au kati ya nchi moja na nchi nyingine  na hii haikuwa Tanzania tu wakati mwingine Tanzania na Zambia na hata wakati mwingine Angola,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo panachangamoto lakini chamoto hizo zimetafutiwa ufumbuzi”. Amesema Prof.Kabudi.

Pamoja na hayo Prof.Kabudi amesema katika mkutano huo pia wameona umuhimu uliopo kwa madereva ambao pamoja na janga hili wameenselea kufanya kazi zao kwani wamewaokoa watu wa kawaida.

Hata hivyo Prof.Kabudi amesema Tanzania inaiunga mkono Kenya kuwa mjumbe asiyekuwa wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri ulitanguliwa  na Kikao
cha Makatibu Wakuu ambao waliandaa nyaraka ambazo zilitumiwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri na kufikia makubaliano hayo.

Mkutano huo umekutanisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara, Uchukuzi, Utalii na Afya kutoka nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Comoro, DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.