Home Mchanganyiko MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA ILANI KWA RC PWANI

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA ILANI KWA RC PWANI

0

Mke wa Rais wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete kulia akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo vitabu viwili ambavyo vina  taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi (CCM) kuanzia kipindi cha  mwaka 2015/2020.

Mke wa Rais wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete kulia akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo vitabu viwili ambavyo vina  taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi (CCM) kuanzia kipindi cha  mwaka 2015/2020.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kushoto akionyesha kitabu chenye taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi wa Chama cha mapinduzi (CCM) Kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2015/2020 ambayo imetekelezwa na Mke wa Rais wa wamu ya nne Mama Salma Kikwete ambaye alikuwa Mbunge wa kuteuliwa.

Mke wa Rais wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete kulia akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kumkabidhi ripoti yake ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha mwaka 2015/2020 

Mke wa Rais wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete wa kati kati akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani kushoto sambamba na wakuu mbali mbali wa idara mara baada ya kumalizika kwa halfa fupi ya kukabidhi vitabu viwili nyenye taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha mwak 2015/2020 ambayo aliitekeleza wakati akiwa Mbunge wa kuteuliwa.(Picha na Victor Masangu

………………………………………………………………………………….

VICTOR MASANGU, PWANI..

 Mke wa Rais  wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete ambaye pia alikuwa Mbunge wa kuteuliwa kupitia Mkoa wa Pwani na Lindi amesema ataendelea kushirikiana bega kwa bega  na serikali katika miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ile  ya kimikakati pamoja na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili wananchi.    

Kauli hiyo ameitoa wakati wa  halfa fupi ya kukabidhi taarifa mbili za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi (CCM) pamoja na kitabu cha maswali na majibu aliyoyauliza wakati akiwa bungeni kwa  Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambapo ilihudhuliwa na wakuu wa  mbali mbali  wa idara ambapo amebainisha kazi mbali mbali  ambazo amezitekeleza katika jamii katika  kipindi chake cha miaka mitatu ikiwemo katika sekta ya afya, elimu,nishati ya umeme pamoja na kutatua changamoto za wananchi.

“Mnamo kwama 2017 Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli aliniteuwa mimi kuwa Mbunge wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  kupitia mikoa miwili ya Lindi pamoja na Pwani kwa hivyo  nimeweza kufanya kazi hii kwa kipindi cha miaka mitatu na siku ambayo Napata taarifa hii kwa kwa kweli nilikuwa nyumbani kwangu nimeka lakini pindi nilipopata taarifahiinilishukuru sana kwa ni ni fursa ya kuweza kuwatumikia wananchi,”alisema Mama Salma Kikwete.

Aidha alisema kwamba katika kipindi chote alichoteuliwa na Rais Magufuli aliweza kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo pamoja na kutatua changamoto mbali mbali ambazo zilikuwa zinawakabili wananchi wa maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani pamoja na Lindi.

Pia alifafanua kuwa baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo aliweza kuweka mipango madhubuti katika masuala ya kuleta maendeleo  katika Nyanja mbali mbali zikiwemo sekta ya afya, elimu, nishati ya umeme pamoja na kutoa elimu kwa wananchi katika mambo mbali mbali ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo.

“Kwa hiyo mimi kama Mke wa Rais wa awamu ya nne napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuniona na kuniteuwa katika nafasi ya Mbunge na mi mi katika kipindi change chote nimeweza kushiriki kikamilifu katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo ikiwemo miradi ya kimikakati  kwa kushirikiana na serikali kwa hiyo nafasi hii kwangu imeweza kuacha  alama kubwa sana,”alisema Mama Salma Kikwete.

Aidha katika hatua nyingine Mama Salma Kikwete amepongeza Rais wa wamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuweza kumteuwa kuwa Mbunge wa Bunge la Muungano wa Tanzania mnamo mwaka 2017  ambapo amedai kwamba kwake ni moja ya heshima kubwa ambayo imeweza kumpa fursa katika utekeleza wa Ilani ya chama cha mapinduzi pamoja na kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta mbali mbali.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amempongeza Mama Salma Kikwete kwa kuweza kushirikiana bega kwa began a serikali ya awamu ya tano katika kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi pamoja na kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo na miradi mbali mbali ya kimikakati.

Pia Ndikilo alimpongeza Mama Salma Kikwete kazi nzuri ambayo aliifanya katika kipindi chote alipokuwa Mbunge wa kuteuliwa na kwamba ripoti ambayo amekabidhiwa ataisoma ili kuweza kuona jinsi ya shughuli mbali mbali alizozifanya na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ilivyofanyika.

                                              

“Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani nampongeza Mke wa rais wa awamu ya nne mama Salma Kikwete kwa kuweza kuja ofisini kwangu na kunikabidhi vitabu viwili ambavyo ndani yake vina ripoti ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 katika ili kwa kweli ameonyesha uzalendo mkubwa na huu ni mfano mzuri wa kuigwa kwa wabunge wa Mkoa wa Pwani na maeneo mengine.