Home Mchanganyiko TAHADHARI KUHUSU WAGONJWA WANAOCHANGISHA FEDHA ZA MATIBABU YA MOYO KWA AJILI YA...

TAHADHARI KUHUSU WAGONJWA WANAOCHANGISHA FEDHA ZA MATIBABU YA MOYO KWA AJILI YA KUTIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) 

0

***********************

Uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) unapenda  kuutahadharisha  Umma kuwa waangalifu na wagonjwa wanaochangisha fedha kwa ajili ya  kutibiwa katika Taasisi hii. Ndugu Mwananchi, inawezekana wagonjwa hao wanaochangisha fedha za matibabu wanakuwa tayari wamepata  msamaha wa matibabu kutoka kwa Taasisi au wasamaria wema wamewalipia.

Kama utakutana na tangazo la aina hiyo kabla hujamsaidia mhusika tafadhali wasiliana  na uongozi wa Taasisi kupitia namba 0222152392/0782-042010/0688-027982 ili kupata ufafanuzi.