Home Mchanganyiko MKURUGENZI WA TAMWA ZANZIBAR APONGEZA JUHUDI NA UBUNIFU WA KIKUNDI CHA MAMBOSASA

MKURUGENZI WA TAMWA ZANZIBAR APONGEZA JUHUDI NA UBUNIFU WA KIKUNDI CHA MAMBOSASA

0

Mkurugenzi wa TAMWA Zanzibar Dr. MZURI ISSA  wakwanza kushoto akiwa na wanakikundi cha Umoja ni Nguvu kilichopom Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba

Uzio wa Banda la Kuku la kikundi cha  Mambo sasa hao,  Mkanyageni kusini Pemba

Wanakikundi cha Mambo sasa Mknyageni Pemba wakiwa katika banda lao la ufugaji wa Kuku lililogarimu shilingi 1,500,000/-

………………………………………………………………………..

Na Masanja Mabula,PEMBA

MKURUGENZI wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar Dk. Mzuri Issa  amepongeza juhudi na ubunifu unaofanywa na wanakikundi cha Mambosasa kilichopo Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba  ambao wameweza kujenga banda la Kuku wao wenyewe na kufanikiwa kuongeza idadi ya Kuku 48 kutoka 20 ambao walianza nao.. 

Dk. Mzuri ametoa pongezi hizo wakati wa Ziara ya kutembelea vikundi vya wajasiriamali kisiwani Pemba kwa lengo la kuona maendeleo ya vikundi hivyo.

Amesema ili vikundi viweze kuimarika zaidi kjiuchumi ni lazima wanavikundi wahamasike  kuchukua mikopo na kutumia mikopo hiyo kujitanua kibiashara na kuongeza uwezo wa kuingiza hisa katika vikundi.

Aidha amlisema katika kuimarisha shughuli za uzalishaji ,kupitia Mradi wa kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Zanzibar (WEZA III), Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar Dk. Mzuri Issa  amewahamasisha wanavikundi kujitokeza kuchukua mikopo kupitia hisa zao ili watanue zaidi biashara zao

“Niwapongeze sana kwa ubunifu wenu mlioufanya, inatia hamasa sana hata kwa wengine,” alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa, “tutumie pia vikundi vyetu kuchukua mikopo ili itusaidie kujiimarisha zaidi kiuchumi.”

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo ameshauri vikundi hivyo kuwatumia wataalamu katika shughuli zao ili waelekezwe namna bora ya kuendesha shughuli zao na kuongeza ubora katika  uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

“Kwasababu Wajasiriamali wengi tunajishughulisha na Kilimo ni vyema kutafuta wataalamu ambao watatuelekeza namna bora ya kufanya kilimo ili kuweza kupata faida inayotokana na bidhaa bora inayozalishwa,” alisema.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Maisha siri, Hadia Hashim Awesu, amesema kupitia vikundi hivyo wamefanikiwa kununua banda lenye thamani ya shilingi Milioni Moja na Laki Tano kwaajili ya ufugaji wa kuku.

“Kupitia miradi midogo midogo tunayojishughulisha nayo kama vile kuuza kuni tumeongeza zaidi mtaji wetu kwa kuchukua mkopo na kupitia hisa zetu tumefanikiwa kupata banda lenye thamani ya shilingi 1,500,000/- kwaajili ya kuendeleza ufugaji wa Kuku.

Katika ziara hiyo Mkurugenzi huyo amefanikiwa kuvitembelea jumla ya vikundi 20   vilivyopo katika Wilaya za Mkoani, Wete na Micheweni Pemba na kushudia mafanikio waliyo yapata wanavikundi kupitia Mradi wa kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Zanzibar (WEZA III) unaotekelezwa na TAMWA Zanzibar  kwa ufadhili wa Milele Zanzibar Foundation.