Home Biashara Huduma ya M-Pesa ya Vodacom Sasa Ulimwengu Mzima

Huduma ya M-Pesa ya Vodacom Sasa Ulimwengu Mzima

0
_AAD7693.JPG
Meneja Msaidizi wa Idara ya Ukaguzi na Sera Benki Kuu ya Tanzania, Albert Cesari (wa nne toka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watendaji wakuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC mara baada ya kuzindua huduma mpya ya kutuma na kupokea pesa kutoka nchi zaidi ya 200 duniani kupitia mtandao wa M-Pesa (Dunia Kijiji na M-Pesa) hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaaam

image.png
Cynthia Ponera – Mkurugenzi Mkazi wa World Remit Tanzania, akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Dunia Kijiji na M-Pesa inayowezesha wateja kutuma na kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 200 duniani kwa kutumia mtandao wa M-Pesa

image.png
Albert Cesari- Meneja Msaidizi wa Idara ya Ukaguzi na Sera Benki Kuu ya Tanzania akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Dunia Kijiji na M-Pesa inayowezesha wateja kutuma na kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 200 duniani kwa kutumia mtandao wa M-Pesa
image.png
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania PLC, Rosalyn Mworia akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Dunia Kijiji na M-Pesa inayowezesha wateja kutuma na kupokea pesa kutoka zaidi ya nchi 200 duniani kwa kutumia mtandao wa M-Pesa
…………………………………………………………………………….

– Zaidi ya nchi 200 zitaweza kutuma na kupokea fedha kupitia M-Pesa                                             – Huduma za fedha kupitia simu za mkononi kuchochea ukuaji wa uchumi Afrika                           

 Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali nchini kupitia huduma ya kifedha ya Vodacom M-Pesa leo imetangaza kuongezeka kwa mfuko wake wa huduma za kutuma na kupokea fedha kimataifa.  Wateja wa Vodacom sasa watakuwa na uwezo na nafasi ya kutuma na kupokea fedha kutoka  kwa wenzao katika nchi zaidi ya 200 duniani kote. 

Jambo hili lilizungumzwa katika siku ya kimataifa ya kutuma fedha kwa familia (international day of family remittances), tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam ambako wadau walikutana kujadili kuhusu hatima ya utumaji wa fedha kimataifa baada ya COVID 19. 

Akizungumza wakati wa majadiliano Meneja Msaidizi Idara ya Usimamizi na sera katika Kurugenzi ya Mifumo ya Kitaifa ya malipo kutoka Benki Kuu Bwana Albert Cesari, alisema serikali imeangalia upya sera zinazosimamia huduma ya malipo nchini ili kuhakikisha huduma na biashara zinaendelea wakati dunia inapambana na mlipuko wa COVID-19.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa M-Commerce wa Vodacom alisema kwamba kutuma fedha kimataifa inawawezesha watu na wafanya biashara wadogo kuendelea kuunganishwa bila kujali mahali walipo. Alibainisha zaidi kwamba utumaji wa fedha kimataifa unaendelea kubadilisha maisha ya maelfu ya watanzania kupitia kuwezesha malipo katika elimu, afya na vitengo mbalimbali vya biashara, kampuni ya Vodacom Tanzania ina nia ya kuendelea kuimarisha mfumo kwa ajili ya Watanzania wanaofanyakazi nje ya nchi ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii jambo ambalo litachangia katika ukuaji wa maendeleo ya nchi kwa ujumla. 

“Tunajivunia kuwa wawezeshaji katika mfumo wa malipo kwa kuwezesha biashara inayohusisha nchi moja na nyingine katika ukanda huu kwa kutuma na kupokea fedha kwa urahisi na bila usumbufu wowote kutoka mahali popote duniani kupitia huduma ya M-Pesa ya kutuma na kupokea fedha kimataifa,” alisema.

Vodacom M-Pesa imeongeza ukubwa wa mfuko wake wa ushirikiano na nchi mbalimbali katika miezi michache iliyopita kwa lengo la kupanua wigo wa huduma ya kuhamisha fedha duniani kote.  Katika ngazi ya kimataifa, washirika wengine wakiwemo MoneyGram, WorldRemit, Remitly na JubaExpress ambao wote hawa watawasaidia wateja kupokea na kutuma fedha kutoka nchi zaidi ya 200 duniani kote moja kwa moja katika akaunti ya M-Pesa.

Ushirikiano katika pembe ya Afrika unajumuisha Safaricom, MTN, EcoCash na Mama Money ambao utawezesha wateja kutuma na kupokea fedha kutoka Kenya, Uganda, Zambia, Burundi na Afrika Kusini. 

“Kutokana na kuwa na mtandao mkubwa wa washirika wa kutuma na kupokea fedha kimataifa, dunia ni kama kijiji kwa M-Pesa. Tunawashukuru wateja wetu kwa ushirikiano wao na tunaendela kuwas makini katika kutimiza maono yetu ya kuiongoza Tanzania kuelekea katika zama za kidijitali na kubadilisha maisha kwa kupitia teknolojia,” alihitimisha.   

Afisa Mtendaji Mkuu wa Thunes bwana Peter De Caluwe alipongeza jitihada hizi na kusema ushirikiano kama huu na ubunifu unaendana na ari halisi ya kiafrika kwa sababu nchi za kiafrika zimeunganishwa siku zote kupitia muingiliano wa watu, bidhaa na huduma.  Huduma ya kuhamisha fedha kimataifa ni muhimu sana katika uchumi wa Afrika kwa sababu unawezesha kuingia kwa fedha za kigeni katika hizi nchi ambazo zina athari ya moja kwa moja katika ustawi wa jamii na uchumi wa waafrika”.  

“Wakati umuhimu wa huduma za fedha kupitia simu za mkononi katika ushirikishwaji wa kifedha katika masoko yanayoendelea ni ya muhimu sana, huduma ya IMT ya M-Pesa inaenda mbali zaidi kwa kuruhusu huduma ambayo hapo awali ilikuwa haipo ya kutuma na kupokea fedha kimataifa na kuifanya kuwa nafuu.  Hivyo ushirikiano wetu na Vodacom M-Pesa una lengo la kuongeza wigo wa kuhamisha fedha kimataifa’.