Home Mchanganyiko ANAEDAIWA KUMUINGILIA KIMWILI MLEMAVU AENDELEA KUSOTA RUMANDE

ANAEDAIWA KUMUINGILIA KIMWILI MLEMAVU AENDELEA KUSOTA RUMANDE

0

******************************

Na Masanja Mabula , Pemba.

ANAYEDAIWA kumuingilia msichana mwenye ulemavu wa akili aendelea kusota rumande baada ya mahakama ya mkoa wa  Kaskazini Pemba imemrejesha hadi tarehe 30 mwezi huu.

Mtuhumiwa anafahamika kwa jina la Juma Mohammed Juma –KIWI-mkazi wa makangale Wilaya ya Micheweni ambaye anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 18/06/2019 majira ya saa tisa jioni.

KIWI alitenda kosa ikiwa ni kinyume na kifungu cha 116(1)sheria namba 6/2018, sheria ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Baada ya mtuhumiwa anayefahamika kwa jina la Juma Mohammed Juma –KIWI-kupanda mahakamani hapo , Mwendesha mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa mashkata Juma Mussa Omar alisema kesi ipo kwa ajili za kusikilizwa lakini naomba uipangie siku nyengine ili mashahidi waitwe.

“Mhe shauri hili liko kwa ajili za kusikilizwa , lakini naomba upange siku nyengine na mashahidi waitwe kuanza kutoa ushahidi wao”alisema.

Hakimu wa mahakama hiyo Abdalla Yahya Shamuhuna aliahirisha kesi hiyo na kutaka siku ya tarehe 30  mashahidi waitwe ili tuanze kuisikiliza.

“Hakikiseheni siku hiyo mashahidi wanafika ,ili tutamilishe upande wa mashahidi na kesi tuitolee hukumu”alisisitiza.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo aliomba apew dhamana akidai kwamba amekaaa rumande kwa muda mrefu.