Home Mchanganyiko AHUKUMIWA JELA KWA MAKOSA MAWILI TOFAUTI VISIWANI PEMBA

AHUKUMIWA JELA KWA MAKOSA MAWILI TOFAUTI VISIWANI PEMBA

0

…………………………………………………………..

Na Masanja Mabula,Pemba.

NYONGEZA huja penye fungu , ndio ambavyo tunaweza kusema baada ya Mahakama ya Mkoa wa Kaskazini  Pemba kumpa adhabu ya kutumikia chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka saba kijana Juma Hamad Ali 30 ambaye alikuwa anatumikia chuo cha Mafunzo kwa kipindi cha miaka miwili.

Kijana huyo ambaye  ni mkaazi wa kijiji cha maambani shehia ya Kiuyu wilaya ya Wete ametiwa hatiani na mahakama hiyo kwa makosa mawili tofauti ikiwemo la kutorosha na kubaka.

Hakimu wa mahakama hiyo abdalla yahya shamuhuna akisoma hukumu amesema , kosa la kutorosha kijana huyo atatumikia chuo cha mafunzo miaka miwili huku kosa la kubaka atatumikia chuo cha mafunzo miaka 5.

Awali mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Juma Mussa Omar ameitaka mahakama itoe adhabu kali kwa muthumiwa kwani matendo hayo yamekithiri ndani ya jamii.

“Mhe Hakimu naomba umpe adhabu kali mtuhumiwa ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hii kwani makosa ya aina hii yamekithiri ndani ya jamii”alisema.

Hati ya mashtaka inaeleza kwamba kijana huyo ametenda kosa hilo tarehe 18/5/2019, huko maambani Kiuyu , ambapo ya halali na ridhaa ya wazee alimtorosha na kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13 jina tunalihifadhi.

Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza tarehe 31 /5/2019  ambapo jumla ya mashahidi saba wamejitokeza kutoa ushahidi na hukumu yake kutolewa leo.

Hata hivyo Mratibu wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Zanzibar-TAMWA –Pemba Fat-hiya Mussa Said akizungumzia adhabu hiyo amesema iwapo mahakama zitaendelea kutoa adhabu kali kama hiyo matendo ya udhalilishaji wa wanawake na watoto yaweza kupungua