Home Mchanganyiko NJIA PEKEE YA KUMUENZI RAIS DKT.SHEIN NI KUKIZAWADIA USHINDI MKUBWA CHAMA CHA...

NJIA PEKEE YA KUMUENZI RAIS DKT.SHEIN NI KUKIZAWADIA USHINDI MKUBWA CHAMA CHA MAPINDUZI-MHE.MARIAM

0

mwakilishi wa jimbo la Gando Mhe Mariam Thani Juma akimkabidhi madawati Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Bopwe Msingi Ali Makame Tani

******************************

Na Masanja Mabula ,Pemba.

MWAKILISHI  wa Jimbo la Gando Mhe Mariam Thani Juma amesema njia pekee ya kumuenzi Rais wa Zanzibar Mhe Dkt Ali Mohammed Shein kutokana na mazuri aliyowafanyia ni kukizawadia ushindi mkubwa chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu.

Akizungumza baada ya kukabidhi madawati katika skuli ya Msingi Bopwe, Mhe Mariam alisema serikali ya Mapinduzi  awamu wa saba imefanya mengi kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundo mbinu ya elimu.

Alisema miaka kumi ya Uongozi wa Dkt Shein Jimbo la Gando limefanya mambo mengi ya maendeleo , hivyo wananchi wanatakiwa kuunga mkono juhudi zake.

“Ni lazima tumuenzi Dkt Shein kwa kukipa zawadi ya ushindi wa kishindo chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu baadae mwaka huu”alisema.  

Akipokea msaada huo , Mwalimu Mkuu wa skuli ya Msingi Bopwe, Ali Makame  Tani alishukuru msaada huo na kusema umekuja kumaliza tatizo la upungufu wa vikalio.

“Tumekuwa na changamoto kubwa ya vikalia katika skuli yetu, hivyo msaada wa leo utasaidia kupunguza tatizo hilo”alieleza.

Akitoa neno la shukrani sheha wa Shehia ya Bopwe Bi Ramia Said Rashid amemshukuru mwakilishi kwa msaada wake huo na kuwataka wananchi kuulinda na kuuthamini.

Jumla ya madawati 60 na viti 180 yamekabidhiwa katika skuli hiyo ambayo yametolewa na Serikali ya Mapinduzi kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Jimbo hilo.