Home Siasa CCM BAGAMOYO YARIDHISHWA NA KAZI YA UTEKELEZAJI WA ILANI ILIYOFANYWA NA MGALU...

CCM BAGAMOYO YARIDHISHWA NA KAZI YA UTEKELEZAJI WA ILANI ILIYOFANYWA NA MGALU KIPINDI CHA MIAKA MITANO

0

****************************

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
Juni 11
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, kimeelezea kuridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani hapo ,Subira Mgalu.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa Alhaj Abdul Sharifu, katika Baraza la Jumuia ya Wanawake (UWT) lililofanyika Msata, ambapo Mgalu na Madiwani wa Viti Maalumu walisoma taarifa za utekelezaji wa kazi zao, katika kipindi cha miaka mitano.
Alieleza,Mgalu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishat, amekuwa akijituma katika kuwatumikia wananchi na Pwani kwa ujumla kupitia nafasi yake ya Ubunge, na kuwahudumia wa-Tanzania kupitia nafasi yake ya unaibu Waziri, huku akimshukuru Rais Magufuli kwa kumteua.
“Chama tunatembea kifua mbele, hii inatokana na kazi kubwa inayofanywa na Mgalu ndani ya Wilaya, Mkoa na mikoa mingine kupitia kofia aliyonayo ya u-Naibu Waziri wa Nishati, ameitendea haki nafasi yake sisi chama tunamuunga mkono kwa asilimia 100,” alisema Sharifu.
Nae Mjumbe wa Kamati ya siasa Wilaya Alhaj Amir Mkang’ata na Katibu Mwenyezi John Fransic “Bolizozo” nao walielezea taarifa aliyoisoma Mgalu imekidhi vigezo, kwani imegusia mambo yote ambayo chama kimeelekeza.
Katika baraza hilo ambalo pia Mgalu alilitumia kukabidhi vyerehani katika kata zote zinazounda Wilaya hiyo, Mwenyekiti wa UWT Bagamoyo, Lukhia Masenga alisema ,wanajivunia kuwa na kiongozi anayejitambua na kuitumikia vema nafasi yake, hivyo wanamuunga mkono katika kazi zake.
Awali akizungumza na wana-UWT hao, Mgalu aliwashukuru wana-Jumuiya na wakazi Pwani kwa namna walivyompatia ushirikiano kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yake, huku akiwatoa hofu wana-Pwani kwamba yeye ni mtumishi wao, hana nia ya kuwania ubunge katika Jimbo.
Katika Baraza hilo Mgalu amelitumia kwa kugawa vyerehani katika Kata zote zinazounda Wilaya, ambapo Jumuia hiyo akiipatia vyerehani viwili vikiwa ni mtaji utaosaidia kujiendeleza kiuchumi, hatimae kuondokana na utegemezi.