Home Mchanganyiko WAFANYABIASHARA MSIWAKIMBIE TRA

WAFANYABIASHARA MSIWAKIMBIE TRA

0

Afisa Msimamizi wa Kodi wa TRA Catherine Mwakilagala aki,fafanu;lia mfanyabiashara jambo

Afisam Msimamizi wa Kodi TRA Isihaka Sharif akihakiki cheti cha Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)

…………………………………………………………………………

Na Oliver Njunwa

Wafanyabiashara katika Mkoa wa Dar es salaam wameshauriwa kutowakimbia maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanapowatembelea katika maeneo yao ya biashara bali watoe ushirikiano ili waweze kufaidi elimu na ushauri unaotolewa na maofisa hao.

Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wafanyabiashara wa Tabata Segerea jijini Dar es Salaam ambao walipata fursa ya kupatiwa elimu wakati wa zoezi la kuelimisha wafanyabiashara katika maeneo yao ya kazi huku wafanyabiashara wengine wakifunga maduka yao.

‘Nimepata mafunzo mazuri baada ya kuwapatia maelezo ya biashara yangu na mapungufu niliyonayo. Wamenielimisha vizuri na kunishauri mambo mazuri kuhusu biashara yangu’, alisema Jamila Mgeni mfanyabiashara wa nguo Tabata Segerea na kuongeza, ‘Mfanyabiashara hana sababu ya kufunga duka au kusingizia kwamba mwenye duka hayupo kwani kufanya hivyo ni kupoteza nafasi ya kuelimishwa”. 

Bi Jamila amesema kwamba endapo mfanyabiashara ana changamoto katika makadirio ya kodi ni vema akakubali kutembelewa na maofisa wa TRA ili wamsaidie na kumuelekeza nini cha kufanya.

Katika hatua nyingine mfanyabiashara huyo aliwasihi wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati ili shughuli ambazo zinafanywa na serikali za kijamii na kiuchumi ziweze kutekelezwa kwa ukamilifu.

Naye Bw. Babin Mohammed mfanyabishara wa nguo za mtumba akasema kwamba kuwakimbia maofisa wa TRA hakuna faida na kuongeza kwamba wanaokimbia inawezekana kuna makosa wanayoyafanya au wana mapungufu hivyo ni vema wakubali kuwasikiliza ili waweze kusaidiwa kwa kuelimishwa na kupatiwa ushauri wa kutatua changamoto zinazowakabili.

Bw. Mohammed amesema kwama yeye mweyewe kuna vitu alikuwa anafanya kimakosa lakini hawakumkaripia bali walimuelewesha kwa utaratibu na kuahidi kufuata ushauri wao.

Akizungumzia zoezi la kuwatembelea wafanyabiashara maeneo yao ya biashara, Afisa Msimamizi wa Kodi Bw. Lameck Ndinda amesikitishwa na wafanyabiashara ambao wanafunga maduka yao na kuwashauri kutoa ushirikiano ili lengo la zoezzi hilo liweze kufanikiwa.

“Lengo la zoezi hili ni kuwaelimisha wafanyabiashara, kufahamu changamoto zinazowakabili, na kupata maoni yao na ushauri kuhusu huduma zinazotolewa na TRA’, alisema Bw. Ndinda.

Kwa mujibu wa Bw. Ndinda uamuzi wa kuwatembelea wafanyabiashara pia ni kuwahamasisha kulipa kodi kwa wakati ili kuwaepusha na adhabu zinazotokana na kulipa kodi kwa kuchelewa.

Amesema kwamba wafanyabiashara hawana  sababu ya kuwakimbia maofisa wa TRA kwani wanapowatembelea wanawapatia ya fursa kuuliza maswali na kuwapatia utaratibu wa kusajili bishara zao wale ambao hawajasajiliwa 

amesema kwamba zoezi hili ni endelevu ingawa  

Zoezi la kutembelea wanfayabiashara katika maeneo yao ya kazi (mlango kwa mlango) ni endelezu na kwa sasa linaendelea katika Mkoa wa Dar es salaam na baadae kuendelea katika mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya na Tanga