Home Mchanganyiko TAKUKURU MANISPAA YA ILALA IMEWATAKA MADIWANI KUTOKUJIHUSISHA NA VITENDO VYA RUSHWA KATIKA...

TAKUKURU MANISPAA YA ILALA IMEWATAKA MADIWANI KUTOKUJIHUSISHA NA VITENDO VYA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO

0

****************************

Na Magreth Mbinga

 

Takukuru Manispaa ya Ilala imewataka Madiwani wa Manispaa hiyo kutokujihusisha na vitendo vya Rushwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu .

Hayo yamezungumzwa na Mchunguzi Mwandamizi Takukuru Ilala Elly Makala kwenye mkutano wa kuvunja Baraza la Madiwani Ilala.

Pia amewaambia Madiwani hao kuwa kazi ya Takukuru ni kuzuia na kupambana na rushwa wasijihusishe na vitendo vya rushwa wakati wa kampeni.

Vilevile Mkuu wa Wilaya ya Ilala DC. Sophia Mjema ameambia Madiwani kuwa Wananchi wana Imani na Serikali yao hivyo waendelee kufanya kazi wasijali kuwa wakati umeisha ili wananchi waendelee kuwaamini wapate kuwachagua tena kipindi kingine.

Sanjari na hayo DC.Mjema amesema Wilaya ya Ilala imekuwa ya kwanza katika ukusanyaji wa mapato kwakuwa kuna umoja na mshikamano na waendelee kuwa na umoja huohuo.

Hata hivyo Meya wa Manispaa hiyo Omary Kumbilamoto amesema Serikali ijayo wanamatumaini makubwa ya kuendelea kuwepo kwenye Baraza hilo na kuwaambia Madiwani yajayo yanafurahisha.

Meya Kumbilamoto amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kwa kumpatia miradi mikubwa mitatu ambayo ni hospitali ya kivule,machinjio ya vingunguti na soko la kisutu