*******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imevunja Baraza lake la madiwani lililohudumu kwa muda wa miaka mitano huku ikikamilisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule tano za sekondari ndani ya Manispaa hiyo.
Akizungumza katika kikao cha kuvunjwa kwa baraza la madiwani katika Wilaya hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe,Benjamini Sitta amesema uongozi wa Manispaa hiyo wa Mwaka 2015-2020 umeweka historia katika nchi hii kwa kutekeleza miradi mingi mbalimbali katika kipindi hicho cha miaka mitano.
“Waheshimiwa mtembee kifua mbele mjue mmeweka historia na rekodi ziko wazi ni halmashauri ya manispaa ya kwanza kuwa na kiwanda cha kuchakata mbolea, kuwa na chuo cha ufundi, kuwa na chuo cha afya chenye ghorofa nne, kuwa hivyo katika nyaja mbalimbali manispaa imeweka historia”. Amesema Mhe.Sitta.
Akizungumza katika baraza hilo Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa Bw. Aron Kagurumjuli amewataka madiwani kuendeleza upambanaji waliouonesha kwa kipindi chote walichofanya kazi ndani ya halmashauri hiyo.
“Hakika uongozi uliopo chini ya Mheshimiwa Benjamini Sitta umeiongoza na kulisimamia vizuri baraza la madiwani na kuleta ufanisi mkubwa”. Amesema Kagurumjuli
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC.Daniel Chongolo amesema kuwa mpaka sasa miradi ya mingi imeweza kutekelezwa katika Wilaya hiyo hasa kwenye miundombinu ya barabara ambapo maeneo mengi yalikuwa ni rahisi kuathiriwa na mvua pindi zinaponyesha.
“Nimefanya kazi na menejimenti ya Mkurugenzi, mnaondoka mkiwa mmeacha safu nzuri sana ya manispaa na yatatekelezwa yale ambayo sisi sasa tunaamini hata yale ambayo mnayaacha hayajakamilika yatakamilika yakiwa salama na ubora unaotakiwa”. Amesema DC.Chongolo.
Amewapongeza Madiwani wa Manispaa hiyo ikiongoza na Msahiki Meya na Naibu wake kusimamia utekelezaji wa irani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye maneneo yenu
“Tunaenda kuendeleza miradi mikubwa ambayo ilikuwa ni muhimu kwenye irani yetu ya Uchaguzi ya 2015-2020 ikiwemo ujenzi wa kumalizia kipande Cha Kisauke kwenda mpaka kule Wazo kiwandani lengo ni kufanya pale katikati Goba mtu awe na option anapoenda Mbweni na Bagamoyo apite kule kwenye rami kutokezea Tegeta na kuendelea na safari”. Amesema DC. Chongolo.