Home Mchanganyiko NKURUNZIZA AFARIKI DUNIA

NKURUNZIZA AFARIKI DUNIA

0

******************************

Rais Mstaafu wa Burundi Pierre Nkurunziza amefariki dunia leo kutokana na mshituko wa moyo.

Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na serikali ya nchi hiyo na kwamba taarifa zaidi kuhusu kifo chake zitaendelea kutolewa.

Nkurunziza amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 55 na alihudumu kiti cha urais nchini humo kwa miaka 15 akiwa Rais wa awamu ya nane kwa tiketi ya Chama cha CNDD-FDD.