Home Mchanganyiko HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAKABIDHI MILION 626 KWA VIKUNDI 100 VYA...

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAKABIDHI MILION 626 KWA VIKUNDI 100 VYA KINAMAMA NA VIJANA

0

MKUU wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro  jana  jijini  Arusha,
akimkabidhi  hundi ya zaidi ya Sh.milioni 626 kwa vikundi 100 vya
vijana,wanawake na watu wenye ulemavu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha
ikiwa sehemu ya fedha za mapato ya ndani ya jiji hilo na marejesho ya
mikopo ya nyuma, ili waboreshe biashara zao picha na Ahmed Mahmoud
Arusha

………………………………………………………………….

Na Ahmed Mahmoud Arusha
MKUU wa Wilaya ya Arusha Gqbriel Daqarro jana amekabidhi hundi ya
zaidi ya Sh.milioni 626 kwa vikundi 100 vya watu wenye
ulemavu,wanawake na vijana ili waendelee kufanya biashara zao bila
kukwama.

Akikabidhi hundi hiyo jana jijini Arusha,alisema fedha  hizo
zinatokana nabmapato ya fedha za ndani za jiji hilo.

“Mikopo hii zamani watu walikuwa hawazipati lakini kutokana na Rais
John magufuli kusema asilimia hii ipelekwe kwa watu wake ndio maana
halmashuri zinatenga na kuwapa wahusika hao,”alisema.

Aidha alisema fedha hizo ziliombwa na vikundi 109, lakini  tisa kati
ya hivyo hazijapata sababu wamekosa sifa, hivyo aliomba wahusika wa
mikopo waelekeze vikundi hivyo ili waendelee kufanya vizuri na awamu
ijayo vipewe kipaumbele.

Aliwataka wanakopeshwa fedha hizo ziwasaidie kukua kiuchumi kwa kupiga
hatua katika biashara zao na kuepuka kuzipeleka kwenye matumizi
yasiokusudiwa.

Pia aliwataka Maofisa Maendeleo Kata kusimamia vizuri vikundi hivyo
pamoja na kuelekeza aina za biashara za kufanya amabzao zitawazalishia
fedha badala ya kuvitelekeza.

“Naomba pia awamu ijayo tuone vikundi vingi zaidi vya watu wenye
ulemavu na tusiwabague ili nao wanufaike na mikopo hiyo na wengi
wakisaidiwa wanaachana na omba omba na wanauwezo wa kufanya
biashara,”alisema.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,  Mwanamsiu
Dossi, alisema fedha hizo zimetokana na urejeshaji wa zaidi ya
Sh.milioni 122.2 wa vikundi vilivyokopeshwa  na zaidi ya Sh.milioni
504.6 zimetokana na fedha za mapato ya ndani.

Alisema mikopo hiyo iliyotolewa  zaidi ya Sh.milioni 626.8 kati ya
hizo Sh.milioni 377 zimetolewa kwa vikundi 65 vya wanawake,Sh.milioni
234.866 vikundi 32 vya vijana na Sh.milioni 15 vikundi vitatu  vya
watu wenye ulemavu.

Alisema halmashauri itaendelea kutoa mikopo hiyo kadiri itakavyokuwa
ikitolewa maombi kutoka kwenye vikundi kulingana na fedha
zitavyopatikana kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani na marejesho
ya mikopo ya nyuma.

Mkurugenzi wa Halmashuri ya Jiji la Arusha Dk.Maulid Madeni amemwomba
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro  kuongeza kiwango cha fedha
za kukopesha kwa walengwa hao ili ziwasaidie kufanya biashara.

“Sio lazima tuwape fedha tunawezabkuboresha kwa kununua mashine za
kufyatulia tofauti vijana na akna mama wapewe mashine za kushona nguo
wakaongeza kipato kwa bidhaa watakazozalisha,”alisema.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Denisi  Zakaria amevitaka vikundi
vya wanawake,vijana na walemavu wanaokopeshwa fedha na serikali
wazirejeshe kwa wakati ili wenzao wapate.
Alipongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuhakikisha asilimia kumi
ya mapato yake ya ndani wanawapa makundi hayo tofauti na
halmashutinzingine nchini wanazitenga na kuzifanyia kazi zingine nje
ya ilivyokudiwa.

“Lakini sababu sisi CCM tuwakuna kwa kuwapa fedha za mikopo nanyi
mtukune wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu,”alisema.