Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI MANYANYA AFUNGUA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MAONESHO YA SABASABA

NAIBU WAZIRI MANYANYA AFUNGUA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MAONESHO YA SABASABA

0

……………………………………………………………………………..

Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella Manyanya afungua rasmi kikao cha maandalizi ya maonesho ya Kimataifa ya Biashara (DITF) ambayo hufanyika nchini mwezi wa saba kila mwaka.
Katika hotuba yake Mhe. Manyanya amepongeza muitikio wa Wizara na taasisi zote zinazohusika katika kuwaunganisha wafanyabiashara ili kukaa na kujadili namna bora ya kuyafanya maonesho ya mwaka huu kuwa bora na ya kisasa.
Mhe. Manyanya ameeleza kuwa mahusiano ya moja kwa moja kati ya Wizara yetu ya Viwanda, Wizara ya mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Kilimo, Wizara nyingine za Kisekta, Taasisi za Serikali na Taasisi Binafsi kutumia fursa ya bidhaa zinazozalishwa na Viwanda vyetu kupata masoko ya ndani na nje kwa bidhaa zetu na kwa kuwa Viwanda ni soko la mazao yanayozalishwa na wakulima, wafugaji na wavuvi.
Mhe, Manyanya ameeleza kuwa dhumuni la kikao hiki kilichoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na TANTRADE ilikuwa ni kuona namna ya kuongeza nguvu ya pamoja hasa katika msimu wa maonesho ya maonesho ya Kimataifa ya Biashara (DITF) kuitumia fursa hii ya maonesho kupata masoko zaidi ya mazao baada ya kuibuka kwa Homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya korona (COVID – 19) ambapo kwa namna nyingine ni fursa kwa wakulima wetu.
Mhe. Manyanya amesema kuwa TANTRADE ina jukumu la kutafuta masoko ya bidhaa zetu zinazozalishwa nchini, hivyo huu ni wakati mahsusi kwa TanTrade kuongeza matumaini kwa wafanyabiashara na wakulima katika kuuza mazao yao baada ya ugonjwa huu kuathiri dunia kiuchumi.
Mhe, Manyanya aliwaagiza wataalamu wote waliokutana kuweka mikakati ya pamoja ya ushirikiano, ili kuhakikisha jambo hili linafanikiwa kama ilivyo dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuifikisha nchi yetu katika uchumi wa Kati wa Viwanda ifikapo 2025.

Wizara nyingine za Kisekta, Taasisi za Serikali na Taasisi Binafsi.
Kwa kusema haya machache, kikao hiki nimekifungua rasmi na ninaamini tutakuwa na mawasilisho na majadiliano yenye tija hususan tunapoelekea katika maandalizi ya maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF).