Home Mchanganyiko MAVUNDE AKABIDHI GARI LA KUSAFIRISHA WAGONJWA KITUO CHA AFYA CHA MKONZE

MAVUNDE AKABIDHI GARI LA KUSAFIRISHA WAGONJWA KITUO CHA AFYA CHA MKONZE

0

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akiwa kwenye gari  gari la wagonjwa(Ambulance) kabla ya kulikabidhi katika kituo cha Afya cha Mkonze Jijini Dodoma.

 

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akizungumza na wananchi pamoja na wahudumu wa afya wakati akikabidhi gari  gari la wagonjwa(Ambulance) katika kituo cha Afya cha Mkonze Jijini Dodoma.

Hilo ndio gari  gari la wagonjwa(Ambulance) lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde  katika kituo cha Afya cha Mkonze Jijini Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akimkabidhi funguo wa  gari  gari la wagonjwa(Ambulance) ambapo ametoa katika kituo cha Afya cha Mkonze Jijini Dodoma.

Diwani wa Kata ya Mkonze Mh David Bochela akitoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde ambaye amekabidhi  gari  gari la wagonjwa(Ambulance) katika kituo cha Afya cha Mkonze Jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde  amekabidhi gari la wagonjwa(Ambulance) kwa ajili ya kituo cha Afya cha Mkonze Jijini Dodoma.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dodoma katika kituo cha Afya cha Mkonze ambapo gari hili litatoa huduma ya usafirishaji wa wagonjwa wa rufaa kutoka katika kituo hicho ikiwa ni ahadi aliyoitoa Mbunge Mavunde wakati wa kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Kituo hicho cha Afya wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018.

“Namshukuru Rais Magufuli kwa ujenzi wa Vituo vya Afya nchini kikiwemo hichi cha Mkonze.Tulikuwa tumebakiza gari tu la wagonjwa na leo tumepata,ni furaha kubwa sana kwamba wananchi wangu sasa watapata fursa ya huduma ya usafirishaji wa wagonjwa tofauti na ilivyokuwa pale awali”

Diwani wa Kata ya Mkonze Mh David Bochela amemshukuru Rais Magufuli kwa ujenzi wa kituo cha Afya cha kisasa ambacho kimerahisisha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi na pia amemshukuru Mbunge Mavunde kwa ufuatiliaji na upatikanaji wa gari hilo ambalo litasaidia kutatua changamoto ya namna ya kuwasifirisha wagonjwa kutoka kituoni hapo kwenda Hospitali ya Rufaa.