Home Biashara NBC YAPONGEZA JUHUDI ZA KOPLO WA JESHI LA POLISI TANZANIA.

NBC YAPONGEZA JUHUDI ZA KOPLO WA JESHI LA POLISI TANZANIA.

0

Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya NBC, Nd. David Raymond akimkabidhi Koplo Brown Twaibu TSHs 1,000,000 kama pongezi kwa juhudi katika kupambana na Covid-19 katika hafla ndogo iliyofanyika katika kituo cha Polisi cha Salander Bridge. Koplo Twaibu alijizolea umaarufu baada ya video yake kusambaa kwenye mitandao yha kijamii akiwahimiza abiria kwenye daladala kufuata maelekezo ya serikali kama kuvaa barakoa ili kujilinda na kuwalinda  na wengine.  Wengine katika picha Kamanda wa Polisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi Zuberi Chembera na Meneja wa Tawi,NBC Mnazi Mmoja Bi. Sada Matitu.

Koplo Brown Twaibu akichapa mwendo kwenda kupokea pongezi ya fedha taslim TSHs 1,000,000 kutoka Benki ya NBC, TSHs 200,000 na cheti cha pongezi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Lazaro Mambosasa iliyowasilishwa na Kamanda Polisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi Zuberi Chembera (wapili kushoto) katika hafla ndogo iliyofanyika katika kituo cha Polisi cha Salander Bridge. Wengine katika picha Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya NBC Nd. David Raymond.

Kamanda Polisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi Zuberi Chembera akipokea salamu kwa ukakamavu kutoka kwa Koplo Brown Twaibu kabla hamjamkabidhi cheti cha pongezi kwa kazi nzuri aliyofanya  katika kupambana na Covid-19. Koplo Twaibu alijizolea umaarufu baada ya video kusambaa akiwahimiza abiria kwenye daladala kufuata maelekezo ya serikali kama kuvaa barakoa ili kujilinda na kuwalinda  na wengine.Wengine katika picha Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya NBC, Nd. David Raymond. na Meneja wa Tawi,NBC Mnazi Mmoja Bi. Sada Matitu.

………………………………………………

Benki ya NBC leo imetambua juhudi mahususi za Jeshi la Polisi Tanzania na maofisa wake katika
kipindi chote cha mlipuko wa homa kali inayosababishwa na virusi vya Covid-19 maarufu kama
corona. Katika matukio mbali mbali ya kipekee, maofisa kwa Jeshi la Polisi Tanzania wameonyesha
hekima ya hali ya juu na dhamira ya kuwatumikia, kuwalinda na kuhakikisha Watanzania
wanatekeleza maelekezo ya wataalam ya jinsi ya kupambana na ugonjwa wa corona.
Aidha, benki hiyo ikishirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania pia imemtambua na kumpongeza Koplo
Brown Twaibu Msoke kwa kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa katika kupambana
na gonjwa la corona. Koplo Taibu alijizolea umaarufu baada ya video ikimuonyesha akiwahimiza
abiria kwenye daladala kufuata maelekezo ya serikali kama kuvaa barakoa, kutosimamisha abiria
kwenye usafiri wa umma na kukaa umbali wa mita moja siyo kwa kujilinda tu bali kuwalinda na
wengine.
Akiongea katika hafla hiyo, Mkuu wa Mawasiliano wa NBC Nd. David Raymond Kigwile alisema
“Kufikia maamuzi ya kumpongeza Koplo Taibu ilikuwa kitu rahisi kwa benki yetu, hususan kwa
sababu vitendo vyake vya kishujaa vinaendana na msimamo wa benki yetu katika kupambana na
virusi vya Covid-19.” Itambulike kuwa Benki ya NBC pia imechukua hatua madhubuti kupamba na
kuenea kwa virusi hivyo kama kuwa benki ya kwanza kuweka vitakasa mikono katika ATM zake
zote nchini, utekelezaji wa nafasi ya mita mbili katika matawi yake. Benki ya NBC pia itaendelea
kuwahamasisha na kuwaelimisha wafanyakazi wake na Watanzania kwa ujumla jinsi ya
kumpambana kwa ugonjwa huyo.
Aidha RPC Ilala Nd. Zuberi Chembera alisema, “Koplo Twaibu ameonyesha mfano mzuri wa
kuhamasisha jamii juu ya uvaaji wa barakoa kwa dhumuni la wananchi kujikinga na kuwakinga
wengine dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona. Kitendo hicho ni mfano wa kuiga na kinahitaji
pongezi ya pekee hususan kipindi hiki ambacho dunia nzima inapambana na janga hili.
Pamoja Benki ya NBC kumtunuku Koplo Brown Msoke fedha taslim TSHs. 1,000,000 na kumfungulia
akaunti katika benki hiyo, Jeshi la Polisi Tanzania pia limemzawadia Koplo Twaibu kiasi cha TSHs
200,000 na cheti maalumu kutoka kwa Kamanda wa Polizi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Lazaro Mambosasa.

Katika kuendeleza dhamira ya kuelimisha jamii matumizi sahihi ya barakoa, Benki ya NBC
imezindua kampeni yake mpya ya #NBCBarakoaChallenge. Pamoja kuhimiza uvaaji wa barakoa,
kampeni ya #NBCBarakoaChallenge itakayoendeshwa kupitia mitandao ya kijamii ya NBC
inaangalia pia kuwakumbusha na kuelimisha Watananzania juu ya umuhimu wa kuzingatia tabia
kinga ili kuzuia Covid-19.
Jinsi ya kushiriki Barakoa Challenge
● Jipige picha ukiwa umevaa barakoa.
● Post kwenye ukurasa wako wa Instagram ukiwa na hashtag #NBCMaskChallenge.
● Watag watu watatu uwaandikie ujumbe wa kuwakumbusha kuvaa barakoa.
Post yenye likes nyingi zaidi kujishindia simu janja aina ya Samsung A10s kila wiki.
Hakikisha akaunti yako haiko private ili tuweze kuona post yako.
Vigezo namsharti kuzingatiwa
Kuhusu National Bank of Commerce