Home Mchanganyiko Atakaye Kwamisha Ujenzi Wa Miundombinu ya HospitaliAswekwe Ndani- Dkt Jasson Rwehikiza

Atakaye Kwamisha Ujenzi Wa Miundombinu ya HospitaliAswekwe Ndani- Dkt Jasson Rwehikiza

0

*****************************

KAGERA

Na Silvia Mchuruza

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt. Jasson Rweikiza ameutaka uongozi wa kata ya Mgajwale katika halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kuwafikisha katika vyombo vya sheria baadhi ya watu wanaokwamisha ujenzi wa hospitali katika kata hiyo.

Dkt. Rweikiza ameyasema hayo kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Kobunshwi na Mugajwale katika kata ya Mugajwale wakati akikabidhi jumla ya Sh.Milioni 2.8 kwa lengo la kusaidia ujenzi wa hospitali ya kata hiyo.

Mbunge huyo ametoa shilingi Mil.1 katika kijiji cha Kobunshwi na shilingi Mil.1.8 katika Kijiji Mugajwale huku akiwataka wakazi wa kata hiyo kuwahoji baadhi ya watu watakaoukuwa na nia ya kugombea ubunge kama kweli wana nia ya kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo.

Kuhusu changamoto ya maji Mbunge huyo ameeleza kuwa serikali ipo katika mchakato wa kufanya usanifu ili kusambaza maji katika kata  sita za Ruhunga,Kyaitoke,Izimbya,Katoro,Mugajwale na Kaibanja sanjari na kukagua ujenzi wa daraja la Kyabalamba ili kujionea hatua za ujenzi wad raja hilo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mugajwale Pastory Kabalende amempongeza mbunge huyo kwa mchango wake katika maendeleo ya kata hiyo huku baadhi ya wakazi wa kata hiyo akiwemo Agnes Simon,Didas Kateme,na Alfunsina Fredrick wakipongeza hatua hiyo kwani wamekuwa wakitembea umbari mrefu zaidi ya kilomita 20 kufata huduma katika kata a jirani za Ruhunga na Izimbya