Home Mchanganyiko MAVUNDE AONGEZA CHACHU KATIKA KUWALINDA WANAFUNZI KUPATA UFAULU MZURI DODOMA

MAVUNDE AONGEZA CHACHU KATIKA KUWALINDA WANAFUNZI KUPATA UFAULU MZURI DODOMA

0

Mbunge wa Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Anthony Mavunde, akizungumza wakati akikabidhi  vifaa kinga kwa shule zote zenye kidato cha sita katika jiji la Dodoma ikiwa ni ndoo na sabuni kwa shule zote za serikali na zile za binafsi.

Sehemu ya vifaa kinga dhidi ya Corona vilivyotolewa na Mbunge wa Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Anthony Mavunde,kwa shule zote zenye kidato cha sita katika jiji la Dodoma ikiwa ni ndoo na sabuni kwa shule zote za serikali na zile za binafsi.

Baadhi ya walimu kutoka shule za Sekondari wakipokea vifaa vya kujikinga na Corona vilivyotolewa na Mbunge wa Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Anthony Mavunde,kwa shule zote za serikali na zile za binafsi zenye wanafunzi wa kidato cha sita ambao leo wameanza masomo.

Mbunge wa Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Anthony Mavunde, akiwa katika picha ya pamoja na walimu pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kukabidhi  vifaa kinga kwa shule zote zenye kidato cha sita katika jiji la Dodoma ikiwa ni ndoo na sabuni kwa shule zote za serikali na zile za binafsi.

…………………………………………………………………………………….
Na. Alex Sonna, Dodoma
Mbunge wa Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Anthony Mavunde, amekabidhi vifaa kinga kwa shule zote zenye kidato cha sita katika jiji la Dodoma ikiwa ni ndoo na sabuni kwa shule zote za serikali na zile za binafsi ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali hasa kipindi hiki ambapo vyuo na shule za za sekondari kwa kidato cha sita wanarejea masomoni.
Katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Mbunge huyo amesema lengo la kukabidhi vifaa hivyo ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira salama hasa kipindi hiki wametoka likizo ndefu na wanakaribia kufanya mitihani yao ya mwisho.
Aidha amesema kuwa Vifaa hivyo ametoa kwa shule zote zenye kidato cha sita zile za serikali na binafsi ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa salama mda wote wawapo shuleni hasa kipindi hiki ambapo dunia inapitia wakati mgumu wa janga la Corona.
“Na vifaa hivi nitakabidhi kwa kila mwalimu mkuu ambapo nitamkabidhi ndoo kubwa(jaba) yenye uwezo wa kuhifadhi maji mengi na ndoo za kawaida nne na sabuni ambazo zitawekwa mahali tofauti katika shule zetu” amesema Mhe. Mavunde.
Mhe. Mavunde amesema kuwa amesukumwa kufanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na janga la Corona, na amewataka wanafunzi wanaorudi shuleni kuzingatia masoma ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona ili wamalize mitihani yao salama.
Pia Mhe. Mavunde ametoa wito kwa wanafunzi wote kusoma kwa bidii ili wafaulu vizuri na kulete sifa nzuri ya jiji la Dodoma na ukizingatia ndio makao makuu ya nchi na serikali katika nafasi yake itafanya kila njia kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.
Naye Afisa Elimu Sekondari Jiji la Dodoma Bi. Upendo Rweyemamu, ameshukuru kupatiwa msaada huo kwa shule zake na kusema itakuwa msaada mkubwa katika kipindi hiki shule zinafunguliwa.
“Ni mshukuru mhe. Mbunge amekuwa msaada sana kwa jamii yake katika jiji la Dodoma na sio leo tu tumekuwa tukishirikiana mara kwa mara na msaada huu utaenda kuwa chachu kwa wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri” ameleza Bi. Upendo.
Kwa upande wake mwakilishi wa wakuu wa shule zenye kidato cha sita kwa jiji la Dodoma Mwalimu Lowael Lyimo, ambaye ni mkuu wa shule ya Maria De Mathias, amemshukuru Mbunge huyo kwa mchango wake katika sekta ya elimu kwa shule zote kwani mda wote amekuwa bega kwa bega na wao katika kuziwezesha shule na hata kuwapa nasaha wanafunzi pindi anapotembelea shule.