Home Mchanganyiko WAZIRI JAFO ATOA SIKU 17 SOKO LA MOROGORO KUKAMILIKA

WAZIRI JAFO ATOA SIKU 17 SOKO LA MOROGORO KUKAMILIKA

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa uongozi wa Manispaa ya Morogoro kukamilisha ujenzi wa soko hilo ndani ya siku 17 ifikapo June 17 mwaka huu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Mhe.Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Loatha Sanare pamoja na baadhi ya viongozi akiendelea kukagua miradi mbalimbali ya Mkoa huo.

……………………………………………………………………………

Na.Mwandishi Wetu,Morogoro
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo ameagiza kukamilishwa kwa ujenzi wa soko la Manispaa ya Morogoro ifikapo Juni 17 mwaka huu.

Agizo hilo amelitoa leo mjini Morogoro katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyo chini ya Ofisi hiyo yake baada ya kuona kuwa limechelewa kukamilika ndani ya muda uliopangwa awali.

”Hili ni Soko  kubwa la bidhaa kupitia fedha za miradi ya kimkakati hapa nchini lilioanza kujengwa mwanzoni mwa mwaka wa jana ambalo litawezesha wafanya biashara kupata mazingira rafiki ya kufanyia biashara”amesema Jafo

Aidha Jafo ametembelea na kujionea  ujenzi wa stendi ya daladala ya Mafiga inayojengwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(Tarura)  kwa ajili matumizi ya Manispaa hiyo ya Morogoro huku akifurahishwa na kazi ya ujenzi wa stendi hiyo ambayo imefikia  wastani wa asilimia 98 ya ujenzi.

Jafo ameitaka Manispaa hiyo kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vikiwemo masoko na standi za mabasi ili kuongeza pato la Manispaa hiyo.