Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

0

………………………………………………………………………….

TAARIFA YA OPERESHENI YA PAMOJA YA MIKOA MINNE

     YA NYANDA ZA JUU KUSINI MBEYA, RUKWA, KATAVI

                                                       NA SONGWE.

Jeshi la Polisi Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya, Rukwa, Katavi na Songwe limefanyika operesheni ya pamoja kuanzia tarehe 17.04.2020 hadi tarehe 24.05.2020 dhidi ya waganga wanaopiga ramli chonganishi @ lambalamba zinazopelekea mauaji, watuhumiwa wa mauaji wanaokodiwa kuua watu kwa kukata mapanga na watuhumiwa wa makosa mbalimbali kama vile wawindaji haramu, wasafirishaji wa dawa za kulevya, wanyang’anyi wa pikipiki [bodaboda],  uvunjaji, wamiliki wa silaha wasio na kibali na uhalifu mwingine.

Katika operesheni hiyo jumla ya kesi ni 300 zilifunguliwa na watuhumiwa 650 walikamatwa kwa tuhuma mbalimbali. Mafanikio ya operesheni hiyo ni kama ifuatavyo:-

MISAKO YA WATUHUMIWA WA MAUAJI.

Jumla ya watuhumiwa 87 wa makosa ya mauaji walikamatwa wakiwemo watuhumiwa wa mauaji yaliyotokea miaka ya nyuma na watafikishwa mahakamani mara tu upelelezi wa kesi hizo utakapokamilika huku sababu zinazotajwa kupelekea mauaji hayo zikiwa ni imani potofu za kishirikina, wivu wa kimapenzi, kujichukulia sheria mkononi, kulipa visasi na migogoro ya ardhi.

MISAKO YA WAGANGA WAPIGA RAMLI CHONGANISHI @ LAMBALAMBA ZINAZOPELEKEA MAUAJI.

Jumla ya kesi 14 zimefunguliwa na watuhumiwa 15 wamekamatwa kwa tuhuma za kupiga ramli chonganishi zinazopelekea mauaji. Sambamba na hilo vifaa mbalimbali vya kupigia ramli chonganishi vilikamatwa yakiwemo matunguli, dawa mbalimbali za kienyeji na Ngozi mbalimbali za Wanyama pori.

MISAKO YA DAWA ZA KULEVYA.

Kwa kipindi tajwa hapo juu, jumla ya kesi 25 za dawa za kulevya zimefunguliwa na watuhumiwa 26 wamekamatwa kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya Heroine na Bhangi. Aidha jumla ya kilogramu 88 na Gramu 92 za Bhangi na Heroine gramu 23.4 zimekamatwa.

MISAKO YA WATUHUMIWA KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.

Jumla ya kesi 16 zimefunguliwa na jumla ya watuhumiwa 24 wamekamatwa kwa tuhuma za kupatikana na nyara za serikali kama ifuatavyo:-

 • Meno matatu ya Tembo yenye uzito wa Kilogramu 5.8 
 • Ngozi moja ya Kobe [Bush baby], ngozi ya nyoka aina ya Chatu [Python], mkia wa Ngiri [Worthog].
 • Nyama ya nyati kilo 20.
 • Mikia 06 ya Nyumbu, Mkia 01 wa Nsha, Mayai 03 ya Mbuni.
 • Mkia 01 wa Ngiri, vipande viwili vya Ngozi ya Chui, Kipande kimoja cha Ngozi ya Nyati.
 • Nyama ya mnyama pori Kuro Kilo 5.2, Nyama ya Twiga Kilo 25, Nyama ya Nyati kilo 20
 • Ngozi vipande 07 pakapori mdogo, vipande 02 vya ngozi ya pakapori mkubwa.
 • Mikia minne ya Nyumbu, ngozi ya Kalunguyeye, mafuta ya Simba, manyoya ya ndege pori.
 • Kucha ya mamba 1, Ngozi ya paka pori. 
 • Mavi ya Tembo na ngozi ya fisi.

MISAKO YA WATUHUMIWA WA WIZI WA PIKIPIKI.

Jumla ya kesi 07 za wizi wa Pikipiki zimefunguliwa, jumla ya watuhumiwa 14 wamekamatwa kwa tuhuma za wizi wa Pikipiki. Aidha jumla ya Pikipiki 11 zimekamatwa kama ifuatavyo:-

 • MC 180 CEK, Sanlg 
 • Pikipiki aina ya King lion isiyo kuwa na namba ya usajili,
 • MC 957 BRS, Boxer
 • MC 645 CHE, King Lion
 • MC.377 CJA, Sanlg yenye fremu namba ljepckl60ka007524 na injini namba 162fmj k7d50090.
 • MC.720 BWY, Kinglion 
 • MC.394 CGW, TVS nakala kumi za kadi za pikipiki zilizogushiwa umiliki zilizokuwa zimetumika kuuzia pikipiki kwa watu mbalimbali na vifaa mbalimbali vya pikipiki.
 • MC 838 CDQ, Boxer  
 • MC 518 CCJ, Toyo 
 • MC 188 AQH, Sanlg 
 • MC 836 BST, Sanlg

MISAKO YA WATUHUMIWA WA UVUNJAJI.

Jumla ya kesi 10 za uvunjaji na wizi zimefunguliwa, watuhumiwa 17 wamekamatwa kwa tuhuma za makosa ya uvunjaji na wizi. Aidha katika operesheni hii mali mbalimbali za wizi toka kwa watuhumiwa zimepatikana:- vifaa vya magari,  mlango mmoja wa gari, Speaker kubwa 2, kinanda cha muziki, amprifire 3, nyaya mbalimbali, vitu mbalimbali mali ya mgahawa wa Zamzam, Microscope student star solar tano (5) na jiko la gas, Sub Woofer aina ya aborder moja, computer aina ya dell moja, cpu moja aina ya hp, mouse moja aina ya hp, taa 04 za solar,  av cable 04, tochi mbili, extension moja, socket moja, usb 09, charger za solar 06, charger za kobe 08, holder 08, cover za simu ndogo 20, card reader 20 na head phone 20. Pia vilikamatwa vifaa mbalimbali vya kuvunjia ambavyo ni nondo 9, mbao 15 na sime 02.

MISAKO DHIDI YA SILAHA ZINAZOMILIKIWA KINYUME CHA SHERIA.

Jumla ya kesi 10 za kumiliki silaha kinyume cha sheria zimefunguliwa na jumla ya watuhumiwa 04 wamekamatwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria. Aidha silaha za aina mbalimbali zimekamatwa katika operesheni hii ambazo ni:-

– SMG A.K 47 mbili zilizofutika namba na magazini mbili na risasi nne.

– Silaha aina ya S/Gun Greener yenye namba 2873.

– Silaha aina ya Gobole Ishirini na Nane [28] zisizokuwa na namba na zimetengenezwa kienyeji na risasi 07 za vipande vya chuma na goroli 142, mitutu minne ya gobore, mideki minne ya gobore na vifaa mbalimbali vya kutengenezea gobole ambavyo ni misumeno miwili ya kukatia chuma, banio moja la kubania chuma, tindo sita, nyundo tatu, mfukuto mmoja utumikao kuchochea moto na tupa nne za kunolea chuma.

Aidha misako dhidi ya makosa mbalimbali imefanyika ambapo jumla ya kesi 42 zimefunguliwa na jumla ya watuhumiwa 65 wamekamtwa kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo kuingia nchini bila kibali, kukamatwa kwa wezi kwa njia ya mtandao, kuingiza nchini bidhaa zilizopigwa marufuku zikiwemo pombe kali, kuingiza nchini bidhaa bila kulipia ushuru, kupatikana na mali za wizi na kupatikana na Pombe Haramu ya Moshi @ Gongo ujazo wa lita 568.5 na Mitambo 03 ya kutengenezea Pombe hiyo.

WITO WA KAMANDA:

Ninatoa wito kwa jamii kuacha kuamini imani potofu za kishirikina, waganga wapiga ramli chonganishi kwani husababisha madhara makubwa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa matukio ya mauaji na ukatili wa kinyama dhidi ya binadamu wasio kuwa na hatia.

Ninatoa wito kwa vijana na jamii kwa ujumla kuacha uhalifu kwani haulipi, ni vyema wakatafuta kazi nyingine ili wajipatie kipato halali kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za kimaisha. Jeshi la Polisi halitakuwa na huruma dhidi ya mhalifu/uhalifu wa aina yoyote, tutaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ikiwa na pamoja na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote.

Aidha ninatoa rai kwa viongozi wa serikali za mitaa na Kata kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Polisi Kata waliopo katika maeneo yao ili kuhakikisha wanazuia uhalifu kwa kuweka mikakati ya pamoja ikiwa ni pamoja na kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi na kuhuisha vilivyopo, kuwafichua wahalifu ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria. Pia ninatoa rai kwa wananchi kutofumbia macho vitendo vya kihalifu, ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola likiwemo Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Mwisho ni rai ya Jeshi la Polisi Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa hatari wa Homa Kali ya Mapafu kwa kuendelea kufuata maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Viongozi Wakuu wa Nchi na Wataalamu wa Afya ili tuendelee kuwa salama.