Home Mchanganyiko MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA SADC NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAANZA

MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA SADC NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAANZA

0

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Agnes Kayola wakati akifungua mkutano wa
Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Maafisa waandamizi wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge akisisitiza jambo kwa wajumbe wa mkutano (hawapo pichani). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Agnes Kayola

Baadhi ya Makatibu Wakuu wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge (wa kwanza meza kuu kushoto) akiongea na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge (aliyevaa koti jeusi) akiongea na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Makatibu Wakuu kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam

*************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge amefungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini DAr es Salaam katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JINCC) kwa njia ya mtandao (Video Conferencing) kuanzia leo tarehe 27 hadi 29 Mei mwaka huu.

Akizungumza katika Mkutano huo Balozi Ibuge amesema kuwa mkutano huo unaanza kwa kukutanisha kamati ya kudumu ya maafisa waandamizi/Makatibu wakuu yeye akiwa kama Mwenyekiti.

Aidha Balozi Ibuge amesema kuwa pia kutawakutanisha na wajumbe wengine ambao ni Prof.Abel Makubi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt.Aloyce Nzuki Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Bi.Amina K.Shaaban Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.

“Mkutano huu pia unajadili hali ya kifedha ndani ya Jumuiya, Utekelezaji wa maazimio yaliyotokana na kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC ambayo ni menejimenti ya Maafa,Utekelezaji wa kaulimbiu ya Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi  na Serikali wa SADC isemayo “MAZINGIRA WEZESHI KWAAJILI YA MAENDELEO ENDELEVU NA JUMUIYA YA VIWANDA, KUKUZA BIASHARA NA AJIRA NDANI YA SADC” na mapitio ya hali halisi ya biashara baina ya nchi , maendeleo ya viwanda ndani ya Jumuiya na taarifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo ya viwanda wa Jumuiya na mpango kazi wake”. Amesema Balozi Ibuge.

Pamoja na hayo nchi zilizoshiriki Mkutano huo ni Angola, Afika Kusini,Comoro,Eswatini,Mauritius,Msumbiji,Madagascar,Namibia,Visiwa vya Shelisheli,Zambia,Zimbabwe na mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.