Home Mchanganyiko BUWASA WAKABIDHI VIZIMBA VYA KUNAWIA MIKONO HOSPTALI YA RUFAA BUKOBA

BUWASA WAKABIDHI VIZIMBA VYA KUNAWIA MIKONO HOSPTALI YA RUFAA BUKOBA

0
Na mwandishi wetu,Bukoba
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA), Wameendelea kurudisha fadhila kwa wateja wao na jamii kwa ujumla kwa kujenga Vizimba Vingine viwili vya kunawia mikono, ikiwa ni tahadhari ya kujikinga gonjwa la corona,na hivyo kufanya Idadi ya vizimba hivyo kufikia vitano vilivyojengwa ndani ya Manispaa ya Bukoba.
Akisoma Taarifa ya utelekezaji wa miradi hiyo, Mkurugenzi wa BUWASA Ndg. John Sirati amesema kuwa Mamlaka katika kuhakikisha jamii inaendelea kuchukua Tahadhari ya Corona, wamendelea kujenga Vizimba vingine viwili vya kunawia mikono kimoja kikijengwa Kituo Kikuu cha Polisi, na Kingine katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Bukoba, na kufanya Idadi ya Vizimba kufikia vitano huku Vizimba kama hivyo vikiwa tayari vimejengwa Stendi kuu na Stendi ya dharula na Soko kuu la Bukoba.
Akizindua Vizimba hivyo, Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora amewataka Wananchi wanaofika maeneo hayo kuendelea kunawa mikono kwani kwa kufanya hivyo, ni kinga ya magonjwa mbalimbali na Corona ikiwa miongoni, na kwamba kunawa mikono na kuchukua tahadhali kutasaidia kujikinga na kuwakinga wengine.
Aidha Profesa Kamuzora amewashukuru BUWASA kwa kuona umuhimu wa kurudisha fadhila kwa wananchi, na kuwaomba wasichoke pale wanapoona kuna uhitaji, huku akisisitiza juu ya huduma zitolewazo na BUWASA huku akidai kuwa wamejitahidi kutoa huduma nzuri hasa kutokatika Maji wakati wote.