Na.Alex Sonna,Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametangaza rasmi kufunguliwa kwa Vyuo vyote nchini na Michezo mbalimbali June 1, 2020 kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa cha Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19).
Pia ameagiza kuwa wanafunzi wa kidato cha sita ambao walikuwa wanatarajia kufanya mithani nao warejee shuleni Juni 1,2020 ili wakamalizie kufanya mitihani yao.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu – Chamwino jijini Dodoma wakati alipokuwa anawaapisha Viongozi mbaliimbali aliowateua hivi karibuni, Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Elimu na Fedha kuhakikisha Wanafunzi hao wa Vyuo wanaorejea Vyuoni humo wanapatiwa Mikopo yao kwa muda mchache uliobaki.
Pia Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Afya kuratibu utaratibu maalum kwa Wanamichezo inaporejea June 1 ili kuhakikisha tahadhari inaendelea kuchukuliwa dhidi ya Maambuzi ya Virusi vya Corona ambavyo vimepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini.
Hata hivyo Shule za Msingi na Sekondari, Dkt. Magufulia ameagiza Shule hizo kujipa muda kidogo kuangalia hali ya Maambukizi ikoje katika kipindi hiki maambukizi hayo yanaendelea kupungua zaidi, “Wanafunzi Shuleza Sekondari na Msingi tuzipe muda kidogo, hawa Wakubwa wanaelewa ziadi kuhusu masuala ya Maambukizi, sisi wa huku tujipe muda kidogo”, amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli ameagiza Mamlaka zinazohusika na masuala ya Utalii kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujio wa Watalii hapa nchini ifikapo May 27-28, 2020 sambamba na kuruhusu Ndege za Watalii hao kutua nchini. “Wakitaka kuja kujifukiza na Nyungu waje tu”, ameeleza Dkt. Magufuli.