Home Biashara TECNO SPARK 5, SIMU YENYE KAMERA 5 KUZINDULIWA IJUMAA HII

TECNO SPARK 5, SIMU YENYE KAMERA 5 KUZINDULIWA IJUMAA HII

0

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO, inatarajia kuzindua simu yake mpya aina ya TECNO SPARK 5 yenye kamera 5 Ijumaa hii kwa njia ya mtandao, ikiwa ni mara ya pili kuzindua kwa njia hiyo ya mtandao ambayo kwa mara ya kwanza ilitanguliwa na TECNO CAMON 15.

Akizungumza kwa njia ya simu leo jijini Dar es Salaam, afisa masoko wa TECNO mtandaoni Bi. Salma Shafii amethibitisha kuwa ni kweli simu hiyo itazinduliwa Ijumaa kwa njia ya mtandao.

“TECNO SPARK 5 ni simu ambayo ina kamera 5 tunatarajia kuizindua Ijumaa hii na imekuja katika wakati muafaka kutokana na kwamba imezingatia ubora, pili imezingatia uchumi wa sasa kwa maana ya bei yake kuwa nafuu sana” Alisema Bi. Salma

Mwonekano wa kamera 5 za TECNO SPARK 5

Kwa upande mwingine TECNO SPARK 5 imekuja ikiwa na betri kubwa yenye kutunza chaji kwa muda mrefu zaidi kutokana na kuwa na 5000mAh. Ni simu isiyohitaji kutembea na power bank” Alisema Bi. Salma.

Hata hivyo TECNO SPARK 5 imethibitishwa kuwa ni simu ambayo ina skrini kubwa yenye inchi 7 na inamwezesha mtumiaji kutazama video au kucheza gemu bila kutatizika na kwa muda mrefu kadiri anavyotaka. Simu hiyo yenye teknolojia ya kisasa kabisa imekuja ikiwa na rangi nne kuu; Ice Jadeite, Spark Orange, Vacation Blue na Misty GreyMwonekano wa pande zote TECNO SPARK 5

Mwonekano wa rangi za TECNO SPARK 5

TECNO SPARK 5 imekuja ikiwa katika aina tatu; SPARK 5 Pro, SPARK 5 na SPARK 5 Air. Ikumbukwe kuwa uzinduzi wa simu hiyo ya SPARK 5 utafanyika katika kurasa za TECNO za mitandao ya kijamii Facebook, Instagram na Twitter tecnomobiletanzania.