Home Mchanganyiko PICHA ZA MAENDELEO YA UJENZI WA VITUO JUMUISHI VYA UTOAJI HAKI (IJC)

PICHA ZA MAENDELEO YA UJENZI WA VITUO JUMUISHI VYA UTOAJI HAKI (IJC)

0

Muonekano wa jengo linalojengwa na Mahakama ya Tanzania la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki   (IJC) lililopo  Jijini Arusha. Jengo  hili  litakuwa na sakafu nne yaani gorofa 3 na yatajumuisha ngazi zote za Mahakama kuanzia Mahakama Kuu mpaka Mahakama ya Mwanzo pamoja na ofisi za baadhi ya wadau wa Mahakama wakiwemo Polisi, Ustawi wa Jamii, Mawakili na Waendesha Mashitaka. 

(Picha na Mahakama ya Tanzania)

Muonekano wa jengo la Muonekano wa jengo linalojengwa na Mahakama ya Tanzania la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) lililopo  eneo Kihonda, Morogoro. Jengo  hili  litakuwa na sakafu nne yaani gorofa 3 na yatajumuisha ngazi zote za Mahakama kuanzia Mahakama Kuu mpaka Mahakama ya Mwanzo pamoja na ofisi za baadhi ya wadau wa Mahakama wakiwemo Polisi, Ustawi wa Jamii, Mawakili na Waendesha Mashitaka. 

Muonekano wa jengo linalojengwa na Mahakama ya Tanzania la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) lililopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Jengo hilo la ghorofa tatu litakuwa na Mahakama ya Mwanzo, Wilaya na Mkoa. Zikiwemo  o ofisi za baadhi ya wadau wa Mahakama wakiwemo Polisi, Ustawi wa Jamii, Mawakili na Waendesha Mashitaka.