Home Mchanganyiko NDEGE YA KWANZA YA WATALII KUTOKA UGIRIKI YATUA  UWANJA WA KIA,ZINGINE KUTUA ...

NDEGE YA KWANZA YA WATALII KUTOKA UGIRIKI YATUA  UWANJA WA KIA,ZINGINE KUTUA  MEI 28 

0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuhusiana n ujio wa Ndege za Watalii na kuanza kwa usafiri wa anga.
………………………………………………………………………………………….

Na. Alex Sonna. Dodoma

Ndege iliyobeba watu saba wakiwemo watalii wanne kutoka nchini Ugiriki imetua leo katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA), ikiwa ni siku chache baada ya serikali kutangaza kufungua anga lake lililokuwa limefungwa kutokana na janga la ugonjwa wa Corona

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa kutokana na kufungua anga leo  majira ya saa 3:30 asubuhi , ndege hiyo ya kwanza imetua na kurejesha usafiri huo.

Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa tayari anayo ratiba ya ndege zingine ambazo nyingi zimeshajaa lakini haswa zitaanza kuja kwa wingi kuanzia Mei 28 mwaka huu.

“Yapo mashirika ya ndege yalishajiandaa kama Emirate, Ethiopia, KLM na kwa upande wa zitakazofanya mizigo tulianza na Rwanda Airline kuanza kubeba minofu ya samaki leo tumeongeza ndege nyingine Ethiopia airline ambayo itabeba tani 19 za minofu ya samaki na Jumapili Ndege hiyo itarudi tena Mwanza kubeba tani 40 ya minofu ya samaki”amesema Mhandasi

Aidha Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa uwanja wa Mwanza ambao nao ni wa Kimataifa umeshafunguka kwa ajili ya kubeba mizigo na wanaendelea na mazungumzo na Waziri wa Mifugo ili waweze kusafirisha pia na nyama.

” Wakati huo huo Ndege yetu ya Tanzania tunakamilisha taratibu kadhaa ili nasi tuanze kuruka kupeleka mizigo Ulaya kwa ajili ya biashara”, ameeleza Mhandisi Kamwelwe.

Mhandisi Kamwelwe ametoa wito kwa watanzania kuona fahari kuwa na Nchi nzuri iliyobarikiwa na Mungu na yenye uongozi wenye maono makubwa chini ya Rais Dk John Magufuli, na kutaka watanzania  kuungana katika kujenga uchumi wa Nchi yetu.