Home Michezo GWAMBINA FC KUWEKA REKODI LIGI DARAJA LA KWANZA

GWAMBINA FC KUWEKA REKODI LIGI DARAJA LA KWANZA

0

Timu ya soka ya Gwambina FC yenye masikani yake Wilayani Misungwi mkoani Mwanza, sasa inasaka pointi tisa katika michezo yake minne iliyosalia ili kufikia rekodi iliyowekwa na Namungo FC ya mkoani Lindi msimu uliyopita. Namungo iliweka rekodi kwa kufanikiwa kupanda daraja kwa alama 49.

Gwambina FC ambayo mpaka sasa ni Kinara katika kundi lake ikiwa na pointi 40 katika michezo 18 huku ikisaliwa na Michezo minne kumaliza msimu. Endapo itashinda michezo yote itaifanya kumaliza ligi daraja kwanza ikiwa na pointi 52 na kupanda daraja kuingia ligi kuu.