Home Mchanganyiko WAANDISHI WA HABARI WA KENYA WALIOINGIA NCHINI KINYEMELA WAKIRI MAKOSA, WALIPA FAINI

WAANDISHI WA HABARI WA KENYA WALIOINGIA NCHINI KINYEMELA WAKIRI MAKOSA, WALIPA FAINI

0

Muuguzi wa Zahanati ya Madizini, Wilayani Mvomero Bi. Eliainenyi Tarimo akijaza taarifa kwenye rejesta ya kliniki ya watoto. Picha na Englibert Kayombo.

**********************************

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Waandishi wawili wa habari kutoka nchini Kenya walioingia nchini Tanzania kinyemela na uanza kufanya kazi bila vibali husika wameburutwa kortini Arusha.

Waandishi hao ambao walishikiliwa baada ya kukamatwa wilayani Longido, wakiwa Mahakamani leo, wamekiri makosa ya kuingia nchini kinyemela na kufanyakazi bila vibali vya kuwaruhusu kufanya hivyo.

Awali makundi ya haki za binadamu yalipiga kelele kuwatetea waandishi hao kabla ya kutulia baada ya Serikali ya Tanzania kushikilia msimamo.

“Leo wamekiri makosa yao na mahakama ikawahukumu kulipa faini ambazo wamelipa na kuachiwa huru,” kimesema chanzo chetu.

Baada ya kuachiwa Mahakamani hapo wawili hao wameongozwa na maofisa wa Tanzania hadi mpakani na kurejea kwao nchini Kenya.