Home Mchanganyiko MBUNGE CHUMI KUTATUA CHANGAMOTO ZA SOKO LA MASHUJAA MAFINGA

MBUNGE CHUMI KUTATUA CHANGAMOTO ZA SOKO LA MASHUJAA MAFINGA

0

Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi  akiongea na wananchi wa jimbo la Mafinga(PICHA KUTOKA MAKTABA)

************************************

NA FREDY MGUNDA,MAFINGA.

WAFANYABIASHARA wa soko la Mashujaa katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga wametakiwa kuendelea kufanya biashara huku kero zao zikiendelea kutatuliwa ili biashara ziendelee kufanyika kwa uhuru na kukuza uchumi wa wananchi wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu kutokea jijini Dodoma,Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi  alisema kuwa amejipanga kuhakikisha anatatua kero ya wafanyabishara hao ili kuendeleza shughuli za kiuchumi kufanyika kwa mujibu wa sheria za nchi.

Chumi alisema kuwa atahakikisha anatatua tatizo la umeme katika soko la Mashujaa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli za kibiashara kwa masaa mengi kama alivyoomba Bungeni kuwa wafanyabiashara wa Mji wa Mafinga wanatakiwa kufanya biashara kwa masaa ishirini na Nne.

“Nikiwa bungeni nilisema kuwa kuna miji ambayo ipo katika barabara ya Daresalaam Zambia na Malawi kufanya biashara kwa masaa ishirini na nne kulinga na taswira ya biashara ambapo kuna mzunguko mkubwa wa fedha katika mazingira hayo” alisema Chumi

Alisema miji midogo kama Mlandizi,Chalinze,Morogoro mjini,Mikumu,ruaha Mbuyuni,Ilula,Ipogolo,Ifunda,Mafinga na Makambako wanatakiwa kufanya biashara kwa masaa ishirini na nne kulinga na kuwa na jografia ya kibiashara.

Chumi alisema anaungana mkono hoja za wafanyabishara wa Mji wa Mfinga kwa kuhakikisha wanafanya biashara masaa ishirini na nne ili kukuza uchumi kwa kasi kubwa kama ilivyo kwa uongozi wa awamu ya tano ambao unawataka wananchi kufanya kazi kukuza uchumi.

Mji wa mafinga ni mji wa kibiashara kama ilivyo kwenye baadhi ya jiji la Nairobi kuna maeneo wanafanya biashara kwa masaa hao ndio maana wanakuza uchumi kwa kasi kubwa hata Mafinga panatakiwa kuwa hivyo.

Chumi alisema wafanyabishara kufanya biashara kwa masaa mengi kunachangia kuongeza kipato hivyo hata ulipaji wa ushuri mbalimbali na tozo zinaongezeka kwenye mapato ya serikali na kukuza uchumi wa nchi.

Aidha Chumi alisema kuwa huduma ya maji na choo ataifanyika kazi licha kuwa uongozi wa soko unatakiwa kuwasilisha maombi kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mfinga ili kuanza kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

Awali wakilalamika wafanyabiashara wa soko hilo la Mashujaa walisema kuwa soko hilo linakosa huduma ya Maji,Umeme,na Choo vitu ambavyo ni muhimu kuwepo kwenye maeneo ya kibiashara kama ilivyo kwenye soko hilo la Mashujaa.

Soko hili linakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa huduma ya ya Choo,Maji na umeme vitu vinavyofanya wafanyabishara wengi kufanya biashara kwa mashaka huku wakiofia afya zao na wateja.