Home Mchanganyiko HEMED AMOUR ANAYEKABILIWA NA KESI YA ULAWITI AMEREJESHWA NA MAHAKAMA YA MWANZO...

HEMED AMOUR ANAYEKABILIWA NA KESI YA ULAWITI AMEREJESHWA NA MAHAKAMA YA MWANZO WETE

0

*************************

Na Masanja Mabua –Pemba.

ANAYEKABILIWA na kesi ya kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 9,amerejeshwa na mahakama ya Mwanzo Wete baada ya hakimu wa mahakama ya Mkoa  anayesikiliza kesi hiyo kutokuwapo mahakamani hapo.

Kijana huyo anayefahamika kwa jina la Hemed Mohammed Amour miaka 20 anadaiwa kutenda kosa siku isiyofahamika mwaka jana huko Daya Mtambwe wilaya ya Wete , mtuhumiwa huyo alimulawiti mtoto wa kiume miaka 9 jambo ambalo ni kosa kisheria.

Akiahirisha kesi hiyo , hakimu wa mahakama ya Mwanzo Wte Maulind Ali Hamad alisema kesi hiyo yenye kumbukumbu namba CC05/2020 ilipaswa kusikilizwa katika mahakama ya Mkoa.

“Kesi hii ipo kwa ajili ya kusikilizwa , lakini mahakama yangu haina uwezo wa kusikiliza kesi za aina hii, hivyo naiahirisha hadi tarehe 18 mwezi ujao ambapo itasikilizwa katika mahakama ya Mkoa”alifahamisha.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka inaeleza kwamba mtuhumiwa huyo alimlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 9 siku isiyofahamika , ambapo ni kinyume na kifungu cha 115(1) cha sheria za adhabu namba 6 za mwaka 2018 sheria za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.