Home Mchanganyiko TANZANIA YAFUNGUA ANGA NDEGE KUTUA NCHINI

TANZANIA YAFUNGUA ANGA NDEGE KUTUA NCHINI

0

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ,azkizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  jijini Dodom wakati akitoa taarifa ya Serikali imetangaza rasmi kufungua anga lake na kuruhusu ndege zote kutua au kupita katika anga la Tanzania.

…………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali ya Tanzania  imetangaza rasmi kufungua anga lake na kuruhusu ndege zote kutua au na kupita katika anga la Tanzania ambalo lilikuwa limefungwa tangu mei 7 mwaka huu kwa kuzuia ndege kutoka nje ya nchi kutua hapa nchini.

Ikumbukwe Mei 7 mwaka huu Tanzania ilitangaza kufunga viwanja vya ndege kuzuia ndege kutoka nje ya nchi kutua hapa nchini ili kuzuia kuenea kwa virus vya Corana.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuanzia leo Serikali inaondoa zuio hilo na kuruhusu ndege zote kutua hapa nchini.

“Baada ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa huo hapa Tanzania kama ilivyoelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jana mai 17, 2020, imebainika kuwa udhibiti wa ugonjwa huo umeendelea kuimarika”

” Kwamba wagonjwa wamekuwa wakipungua katika vituo mbalimbali vya afya nchini hivyo Serikali inatangaza kufungua anga lake rasmi kuanzia leo tarehe 18, mei, 2020″ amesema Kamwelwe.

Amesema kuanzia sasa ndege zote za kibiashara, misaada, kidiplomasia , dharura na ndege maalumu zinaruhusiwa kuruka, kutua, na kupita juu ya anga la Tanzania kama ilivyokuwa awali.

Aidha Mhandisi Kamwelwe amebainisha kuwa taratibu za kiafya zilizowekwa na shirika la afya ulimwenguni (WHO) pamoja na Wizara ya Afya zitazingatiwa wakati wote.

Amesema watahakikisha abiria wote ingia na kutoka watapimwa joto na endapo watahisiwa kuwa na viashiria vya virus vya Corona watawekwa sehemu maalumu kwa ajiri ya uchunguzi zaidi.

Pia ameagiza mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA) kuliarifu Shirika la anga la kimataifa kuhusu maamuzi haya na kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa bila vikwazo vyovyote.

Pia amezitaka mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) pamoja na Kampuni ya kusimamia na kuendeleza uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro ( KADCO) kuhakikisha wanajipanga vyema kuhudumia ndege mbalimbali zitakazoingia nchini ikiwa ni pamoja na ndege zitakazobeba watakii.