Home Mchanganyiko MZEE WA MIAKA 94 ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA...

MZEE WA MIAKA 94 ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 14 VISIWANI PEMBA

0

……………………………………………………………………………….

Na Masanja Mabula ,Pemba..

MZEE mwenye umri wa miaka 94 mkaazi wa kisiwa cha Fundo katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14.

Mzee huyo anayefahamika kwa jina la Abeid Juma Abeid 94 anadaiwa kutenda kosa hilo tangu mwanzoni mwa mwaka huu ,baada ya wazazi wa moto huyo kuwa safirini.

Akithibitisha kukamatwa Mzee huyo Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Kaskazini Pemba , Kamishna Masaidizi Mwandamizi Juma Sadi Khamis alisema upelelezi unaendelea na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

“Tunamshikilia mzee Abeid Juma Abeid (94)kwa tuhuma za kumbaka mtoto  wa kike mwenye umri wa miaka 14, tunamhoji na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili pindi upelelezi ukikamilika”alifahamisha.

Aidha Kamanda Sadi aliwataka wananchi kuwa karibu na watoto wao pamoja na kufuatilia meenendo yao.

“Niwoambe sana wazazi na walezi kuwa kaaribu na watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia mienendo yao , jambo ambalo litasaidia kuwalinda dhidi ya vitendo vya udhallishaji”alisisitiza.

Afis usitawi wa Jamii Wilaya ya Wete Haroub Suleiman alisema licha ya wazazi wa mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho kushindwa kutoa ushirikiano, lakini mtuhumiwa atashitakiwa na Jamhuri.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni wiki mbili zimepita katika kisiwa hicho , kuripotiwa tukio la mzee haroub ali kombo  75 kushatikiwa na mzee mwenzake Ofisi  ya Mkuu wa Mkoa huo kwa tuhuma  ya kuiba mke wa mtu.