Home Mchanganyiko WANANCHI ARUMERU WAISHUKURU SERIKALI

WANANCHI ARUMERU WAISHUKURU SERIKALI

0

………………………………………………………………………………..

Na Mwandishi Wetu, Arumeru

WANANCHI wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, wameishukuru Serikali kwa kuwaandalia utaratibu wa kupata sukari iliyokuwa imeadimika.

Wakitoa Shukrani hizo, wakati wakipokea sukari katika zoezi la awamu ya pili ya ugawaji wa sukari, baadhi ya wananchi hao walisema sukari hiyo imekuja wakati muafaka hasa kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani.

Wamempongeza waziwazi Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro, kwa hatua yake ya kuwapambania katika matatizo mbalimbali Ikiwemo Suala hilo la sukari.

“Pamoja na kuishukuru serikali, lakini tunampongeza mkuu wetu wa wilaya Jerry Muro kwa kusimamia vema zoezi la ugawaji sukari, alisema mmoja ya watu waliofika eneo la ugawaji huo.

Naye Mkuu huyo wa wilaya, alisema atasimamia zoezi na kuhakikisha sukari Itafika katika maeneo yote ya Wilaya hiyo ili wananchi waipate kwa bei elekezi.

“Tutahakikisha kila mwananchi anafikiwa na sukari hii katika maeneo yote ya Wilaya yetu, “alisema na kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuhakikisha upatikanaji wa sukari hiyo.

Muro alisema hadi sasa tayari wamegawa kiasi cha mifuko 1,085 katika maeneo mbalimbali katika kukabiliana kile kilichoitwa uhaba wa sukari.