Home Mchanganyiko UTEUZI WA WAKURUGENZI WA MAMLAKA ZA MAJISAFI NA USAFI WA

UTEUZI WA WAKURUGENZI WA MAMLAKA ZA MAJISAFI NA USAFI WA

0

***************************************

MAZINGIRA – ARUSHA NA SUMBAWANGA

 
Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amefanya uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za Arusha na Sumbawanga
kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia leo tarehe 15 Mei, 2020.

Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo imewataja walioteuliwa kuwa ni Mhandisi Justine Gordian Rujomba anayekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), na Mhandisi Gibon Nzowa anayekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Sumbawanga (SUWASA).

Uteuzi huo umefanyika chini ya Sheria Namba 5 ya Usambazaji Maji Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019. Aidha, Wakurugenzi walioteuliwa watakuwa Makatibu wa
Bodi za Wakurugenzi katika mamlaka hizo.