Home Mchanganyiko SHILATU ASHIRIKI UJENZI OFISI YA KIJIJI ”WANANCHI WAFURAHIA”

SHILATU ASHIRIKI UJENZI OFISI YA KIJIJI ”WANANCHI WAFURAHIA”

0

……………………………………………………………

~ Akemea hujuma na tamaa ya posho

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ameshiriki pamoja na Wananchi kwenye ujenzi ofisi ya Kijiji cha Mwenge A kilichopo kata ya Kitama kwa kumwaga zege jamvi.

Gavana Shilatu alijumuika na Wananchi hao ambao walikuwa na kiu ya siku nyingi ya kupata ofisi ya Kijiji chao na hatimaye limewezekana kwa ushirikiano mkubwa wa Afisa Tarafa huyo.

Gavana Shilatu aliwasisitiza Wananchi kuwa Wazalendo na kuacha tamaa ili malengo ya mradi wa ujenzi huo yatimie.

“Kiu yenu ya muda mrefu tumeifanyia kazi na leo ujenzi unaanza, nimefurahi kuona Wananchi walio wengi wakijitoa kujenga na hata usimamizi. Nawasihi acheni tamaa ya kutaka posho ama ya udokozi wa vifaa vya ujenzi. Simamieni mradi wa ujenzi huu wa maendeleo ujengwe kwa haraka na kwa viwango vinavyoendana na thamani ya fedha. Narudia tena ujenzi huu ni kwa faida yenu hatutavumilia Mambo ya hovyo, hatua kali zitachukuliwa.” Alisisitiza Gavana Shilatu.

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji Kijiji cha Mwenge A, Halmashauri ya Serikali ya Kijiji pamoja na kamati ya ujenzi.