Home Mchanganyiko KIJANA ANAYEDAIWA KUMUINGILIA KIMWILI MLEMAVU WA AKILI BADO ANASOTA RUMANDE

KIJANA ANAYEDAIWA KUMUINGILIA KIMWILI MLEMAVU WA AKILI BADO ANASOTA RUMANDE

0

*********************************

Na Masanja Mabula –Pemba.

ANAYEDAIWA kumuingilia msichana mwenye ulemavu wa akili bado anaendelea kusota rumande baada ya hii leo mahakama ya Mwanzo wete kumrejesha rumande.

Kijana huyo anayefahamika kwa jina la Juma Mohammed Juma (Kiwi) 18 mkaazi wa shehia ya Makangale Wilaya ya Micheweni amerejeshwa rumande hadi juni 18 mwaka huu.

Hakimu ya mahakama ya Mwanzo Wete Maulid Hamad Ali amemrejesha rumande mtuhumiwa huyo kutokana na hakimu wa mahakama ya Mkoa anayesilikiza kesi hiyo kuwa  nje ya mahakama kikazi.

Mbele ya Hakimu wa mahakama ya Mwanzo wete Maulid Hama Ali , mwendesha mashtaka wa Polisi Fat-hiya Ramadhan aliiomba mahakama iipange siku nyengine kwa ajili ya kuja kusikiliza kesi hiyo.

“Shauri lipo kwa ajili ya kusikiliza , lakini kutokana na Hakimu wa mahakama ya Mkoa aliyepaswa kusikiliza kesi kutokuwa ,naomba upangiwe siku nyengine”alishauri.

Kwa mujibu wa hati ya mashataka  inasema kwamba Mtuhumiwa huyo alitenda kosa siku ya tarehe 18/11/2019 majira ya saa tatu asubuhi ambapo alimuingilia msichana mwenye umuri  wa miaka 17 ambaye ni ulemavu wa akili.

Mtuhumiwa huyo amerejshwa rumande hadi juni 18 mwaka huu kesi hiyo itakapo rejea kwa ajili za kusikilizwa katika mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyoko Wete.