Home Mchanganyiko KANISA LAINGIA KATIKA IBADA YA SIKU TISA KUMUOMBA MUNGU AMFICHE RAIS DK....

KANISA LAINGIA KATIKA IBADA YA SIKU TISA KUMUOMBA MUNGU AMFICHE RAIS DK. MAGUFULI DHIDI YA WAOVU

0
Rais Dk. Magufuli
**********************

TEGETA, Dar es Salaam

Kanisa la Halisi la Mungu Baba lililopo Tegeta jijini Dar es Salaam, limeingia katika ibada ya siku tisa kumuombea Rais Dk. John Magufuli, Mungu amfiche ili waovu wasimdhuru na ampe maisha marefu ili endelee kuwatumikia Watanzania kwa hekima, busara na maarifa.


Akizungumza jana katika ibada hiyo ambayo ilianza siku sita zilizopita, Kiongozi wa Kanisa hilo anayejulikana kwa jina la Baba wa Uzao aliwaambia waumini kwamba Kanisa limechukua hatua ya kumuombea Rais Dk. Magufuli kwa kuwa linatambua kwamba kutokana na utendaji wake ikiwemo msimamo wake katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona wapo watu aovu ambao wanamuonea donge na kujitafuna vidole kwa hasira.


“Kwa nini tumwinue Rais Dk. John  Pombe Joseph Magufuli kwa Malango tisa (siku tisa)? Mbona tunafanya hivyo kwa siku nyingi kiasi hicho; Kwani kuna nini? Kuna mambo makuu matano ambayo yamesababisha tuombe kwa jinsi hivyo”, alisema Baba wa Uzao na kutaja sababu hizo tano. 


“Jambo la kwanza ni msimamo wake wa kupeleka Wananchi wote kwa aliyetuumba sote, ambaye ni Mungu Baba. Mataifa yote yamehimiza Corona aabudiwe badala ya Mungu kuabudiwa! Kuna ambao walifikia hatua ya kupiga Wananchi wao walioonekana wanaenda kwenye nyumba za ibada. Yeye (Rais Dk. Magufuli akasema jibu la kweli lipo katika kumbkimbilia aliyetuumba sote ambaye anawea kila kitu na ni zaidi ya Corona.


Matokeo ya Rais Dk Magufuli kusema hivyo, ni Tanzania kushambuliwa na baadhi ya Mataifa kwa kutumia vyombo vyao vya habari! Yako Mataifa hawaakufunga mipaka na kuna wagonjwa wengi wa Corona  hawawasemi, badala yake inasemwa Tanzania tu! Jambo hili linatukumbusha kilichoko 2 Mambo ya nyakati 20:1-26.”, alisema Baba wa Uzao na kunukuu kifungu cha maandiko hayo akisema;


“Katika mistari hii Mfalme Jehoshefati alivamiwa na Mataifa matatu, yeye akiwa taifa moja tena dogo. Mfalme Josephati aliita taifa zima kuwaeleza kilichotokea. akiwa kwenye mkutano wa hadhara akijiuliza aanzie wapi kutoa hotuba, ndipo sauti ya Nabii ilisikika katikati yao ikisema ‘Enyi watu wa Yuda na Jehoshefati Mfalme, msiogope maana hii vita si yenu bali ya Mungu Baba’. Mfalme Jehoshefati aliposikia ile sauti alifurahi na kusema kuwa watu wa Yuda wasikilize Sauti ya Nabii ili wafanikiwe na wasikilize sauti ya Mungu Baba ili Wathibitike katika vita yao.


Mfalme Yehoshefati aliamua kuweka wanaoimba kwa uzuri na utakatifu, baada ya kujua kuwa  vita ile si yake wala wananchi wake.  Kilichotokea wale maaduni wote waligeukiana na kukatana mapanga wao kwa wao, ikawa shangwe, nderemo na vifijo kwa upande wa Mfalme Yehoshefati”. 


“Halikadhalika, Tanzania na Rais Dk. Magufuli tufurahi sote maana hii vita ya kuishambulia Tanzania na yeye mwenyewe si yetu nali ni ya Mungu Baba. Wote walioinuka kuishambulia Tanzania au kumshambulia Rais Magufuli, watakatana mapanga wao kwa wao tukiwa tunaona kwa macho yetu”. alisema Baba wa Uzao.


Alisema sababu ya pili ya kufanya maombi hayo ni Rais Dk. Magufuli kumtanguliza Mungu Baba kabla ya kitu chochote.


“Jambo la Pili, Rais Dk. Magufuli anamtanguliza Mungu Baba kabla ya kitu chochote. Sisi sote ni mashahidi, anapoapisha kiongozi yeyote; awe Waziri, Katibu Mkuu, Mkuu wa mkoa au Mkurugenzi na kadhalika huwa lazima  ‘MTANGULIZENI MUNGU BABA’. Hakuna Rais au mtu wa nafasi yake popote ambaye hufanya hivyo! Maana  yake nini?


Tulikuwa tumetawanyika mno, kila mtu na madhehebu yake na kamungu kake! Yeye Rais Dk. Magufuli amegengeneza familia moja kwa kutuelekeza sote turudi kwa aliyetuumba. Hata wale wakorofi, amewaambia  wanakula, wanakunywa, wanaenda chooni na kupumua kwa nguvu ya Mungu Baba wasiomtaka! Katika majira zote na vizazi vyote vilivyopita, kila anayefanya kama Rais Magufuli alikuwa anachukiwa mno”, 


Hata kama hawajitokezi waziwazi, wapo ambao wanauma vidole kwa chuki na hasiara kuwa kwa nini Rais Dk. Magufuli atupeleke kwa Mungu Baba?”,  alisema Baba wa Uzao na kuendelea kusema kuwa;


“Mfano mzuri ni Yesu, zaidi ya miaka 2000 iliyopita, walimpeleka msalabani kwaa sababu ya kusema “Mimi naenda kwa Baba”. Dunia huwa haitaki anayemwinua Mungu Baba. Wanataka ambaye anainua Waganga, Wachawi, Wanajimu na wanaosema dua mbaya hivyo ni lazima tumwinue Rais Dk. Magufuli awe juu ya hao waovu wanaomchukia aliyetuumba sisi sote”.


Akitaja sababu ya tatu ya maombi hayo, Baba wa Uzao alisema, ” Rais Dk. Magufuli ameondoa utumwa wa fikra ambao tulikuwa nao kuwa Watanzania hatuwezi kuendelea bila misaada! kule zamani, nyota ya Tanzania ilikuwa inafanya kazi katika Mataifa mengine ambayo tunayaona yako juu kimwili. Nyota hiyo ilikuwa inachukuliwa kila tunapoabudu watu wengine walioumbwa kama sisi tulivyoumbwa”. 


“Katika Warumi 2:9-10 Kitabu kinaonyesha wazi kuwa hata kama wewe ni mbaya, Kama unatoa msaada kwa mwingine, basi utapata Amani, utukufu na heshima. Jambo hili lilisababisha Nyota ya Taifa Baba yaani Tanania, ikawa inapeleka vitu vizuri kwa wengine ambao siyo kusudi la Mungu Baba. 


Si rahisi kupata Kiongozi wa kutukomboa kifikra jinsi hii ya Rais Dk. Magufuli, ili kiongozi kiongozi huyu awe salama lazima tumwinue juu ya waovu wote ambao hawataki aliyerudisha nyumbani nyota ya Tanzania, Mungu Baba yuko juu ya kila kitu, tukimwinua Rais Dk. Magufuli, hayo mabay kinyume na taifa yanayeyuka”, alisema Baba wa Uzao katika mahuri ya maombi hayo kwa Rais.


Kwa upande wa sababu ya Nne ya kufanya maombi hayo, Baba wa Uzao alisema; “Ni Moyo wa Baba katika Taifa hili la Tanzania. Kwa mujibu wa 1Yohana 5:8, kuna Baba Mwana na Roho. Kitabu kinaonyesha kuwa aliyeanzan kuja juu ya Nchi ni Mungu Roho (Mwanzo 1:2). Wapili alikuwa ni Mungu Mwana (mathayo 2:1-14). na Watatu ambaye ni Mungu Baba alikuwa hajaja. Katika 1 Wakorintho 15:24 iliandikwa kuwa akili ya mtu ukifika mwisho ndipo atakuja Mungu Baba akabidhiwe, Ufalme, Nguvu, Utawala na Mamlaka.


Mataifa mengi yalijua jambo hili nao wakajiandaa kumpokea ila hawakutufundisha hilo jambo. Amerika ilisubiri, Ulaya ilisubiri, Asia ilisubiri, Australia ilisubiri, New Zealoand ilisubiri na kwa Afrika (Ningeria, South Afriva nakadhalika) walisubiri. Sasa Moyo huo wa Baba umeshukia Tanzania na Rais Dk. Magufuli ameonekana kila mahali kuwa Moyo huo wa Mungu Baba. Tunathibisha hayo  kutokana na utendaji alio nao wa kumpenda Mungu Baba kupita kawaida”.


Baba wa Uzao aliongeza kuwaambia waumini katika maombi hayo akisema; “Mataifa yaliyokuwa yanasubiri kumpokea Mungu Baba hawapendi kuona Taifa la Tanzania ambalo lilionekana kuwa chini sasa kuwa juu. Kwa sababu hiyo ni lazima wote tumwinue Rais Dk. Magufuli ili Mungu Baba amfiche, waovu wasimdhuru”.


Kuhusu sababu ya tano ya maombi hayo, Baba wa Uzao alisema, “Ni wale wanaompenda Rais Dk. Magufuli bado wana ufahamu wa Mwana badala ya ufahamu wa  Mungu Baba ambaye amekuja juu ya Nchi. Nimefundisha  kwa kutumia barabara (njia) ya kuandika Makala mbalimbali kwenye Magazeti, kuonyesha jinsi majira ya mwana ilivyoisha na jinsi Majira ya Mungu Baba ilivyokuja kupitia Tanzania.


Kweli ni hii, ukimwinua Rais Dk. Magufuli kwa jina la mwana wakati majira ya mwana imekwisha utalaumu badala ya kupokea thawabu, maana Rais Dk. Magufuli anaongoza awamu ya tano ya Taifa Baba, ambayo kwa mujibu wa Daniel 7:22 inaonyesha kwamba Awamu ya Kwanza iliyoongozwa na Mwalimu Nyerere ilikuwa ya Nabii Musa, Awamu ya Pili iliyoongozwa na Alhaj Ali Hassan Mwinyi ilikuwa ya Nabii Eliya Mtishbi, Awamu ya tatu iliyoongozwa na  Mh. Benjamin Mkapa ilikuwa  ya Yesu, Awamu ya Nne iliyoongozwa na Dk. Jakaya Kikwete ilikuwa ya Adamu wa Pili ambaye ni Nabii wa mwisho.


Hivyo awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, kwa mujibu wa Kitabu cha Daniel 7 ni ya Mungu Baba, Ndiyo Kanisa Halisi la Mungu Baba limejitambua na kumwinua Rais Dk. Magufuli kwa jina la Mungu Baba ambaye ndiye mwenye Majira inayotawala ndani ya Uumbaji wote sasa hivi, kwa hiyo wote wanaompenda Rais Dk. Magufuli, wamwinue kwa jina la Mungu Baba ndipo watapata tahawabu kubwa”.


“Unapomwinua Rais Dk. Magufuli, lazima ujue vita hii siyo suala la Corona, bali ni suala la kumchukia Mungu Baba aliyeshuka Tanzania. Dunia hawamtaki Mungu Baba, wanataka kitu kingine, yeye Rais Dk. Magufuli anajua Mungu Baba ni Mkuu kuliko. Tumwinue Rais Dk. Magufuli ili Mungu Baba amfiche, waovu wasimfikie”, alisema Baba wa Uzao.