Home Mchanganyiko NAIBU MEYA MANISPAA YA UBUNGO AKABIDHIWA OFISI YA MSTAHIKI MEYA

NAIBU MEYA MANISPAA YA UBUNGO AKABIDHIWA OFISI YA MSTAHIKI MEYA

0

……………………………………………………………………………………..

 Naibu Meya Manispaa ya Ubungo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Manzese kupitia chama cha wananchi (CUF) Mhe.RAMADHANI KWANGAYA amekabidhiwa ofisi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic kukaimu nafasi ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo.

Tukio hilo limefanyika mbele ya waheshimiwa Madiwani na wakuu wa Idara na vitengo.

Sambamba na hilo Naibu Mstahiki Meya amekabidhiwa gari kwa ajili ya matumizi ya shughuli zake za kiofisi.

Wakati wa kukabidhi Ofisi hiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo BEATRICE DOMINIC alimkabidhi Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na kanuni za Halmashauri kama nyenzo zitakazomsaidia kutekeleza majukumu yake ya kila siku.