Home Mchanganyiko MKUU WA WILAYA YA MULEBA AREJESHA TABASAMU LA WAKAZI WA KATA ZA...

MKUU WA WILAYA YA MULEBA AREJESHA TABASAMU LA WAKAZI WA KATA ZA KAGOMA NA KIKUKU

0
……………………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango atatua tatizo la kukatika kwa umeme ndani ya siku tatu katika kata za Kagoma na Kikuku wilaya ya Muleba.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Mhandisi Ruyango kuona chapisho la Bw. Omary Rwakyaya la tarehe 8.05.2020 katika mtandao wa kijamii wa Face book likieleza tatizo la kutokuwepo kwa huduma ya umeme kwa wakazi wa kata hizokwa kipindi cha takribani miezi miwili huku sababu ikitajwa kuwa ni kuharibika kwa transfoma iliyopigwa radi katika kata hizo.
Mhandisi. Ruyango baada ya kuona chapisho hilo alitoa maelekezo kwa TANESCO wakishirikiana na REA kuhakikisha wananchi wa kata za Kagoma na Kikuku wanarejeshewa umeme ili kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku ambapo wengi wao wanategemea nishati hiyo kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake mchapisha andiko hilo katika mitandao wa kijamii wa Face book Bw. Omary Rwakyaya ametoa wito kwa viongozi wa kata za Kagoma na Kikuku kuhakikisha wanafikisha matatizo ya wananchi wao kwa mamlaka husika ili yapate kutatuliwa kwa haraka.
“Uwakilishi wa wananchi ni kujitoa na kuguswa na matatizo yao, tusiwe viongozi wa muda mwingi huku tunashindwa kusukuma agenda za wananchi wetu” ametoa rai Bw. Rwakyaya.
Bw. Rwakyaya ameongezea kusema kuwa anawashukuru Mhandisi Ruyango na watendaji wake kwa kutekeleza Majukumu yao kwa ufanisi kwa kuwatumikia wananchi hasa wananchi wa kipato cha chini kama ambavyo imekuwa azma ya serikali chini ya Uongozi Madhubuti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Joseph Magufuli kuhakikisha maeneo mengi ya vijiji yanapata nishati hii ili kuwakwamua wananchi kiuchumi.